Morogoro: Mama agoma mwanaye asizikwe, ataka mwili upelekwe kanisani aombewe ili afufuke

Morogoro: Mama agoma mwanaye asizikwe, ataka mwili upelekwe kanisani aombewe ili afufuke

Hawa manabii feki wameharibu sana watu, hususani akina mama. Kuna mama mmoja aliugua brucellosis kama ilivyo bainishwa na madaktari, lakini ndg wa huyo mama hususani mama yake mzazi na dada yake mgonjwa walikataa katakata huyo mama kutibiwa hospital wakadai wampeleke kwa Mwamposa ili aombewe apone. Kidogo huyo mama akate kamba. Bahati nzuri mgonjwa alijiongeza na kurudi kuendelea na dawa za hospital, hadi sasa ni mzima wa afya.
Mungu katuumba na akili na utashi kusudi tuweze kukabiliana na changamato tunazokutana nayo.

Unajua kabisa haya ni Malaria na dawa zake unazijua na pesa mfukoni unazo hutaki kutumia unataka kuombewa. Kama sio kumjaribu Mungu wako ni nini?
 
Wakuu

Hali ya sintofahamu imeibuka eneo la Forest Hill, mjini Morogoro baada ya kifo cha binti Irene Joseph Akaro (30), ambapo mama wa marehemu ametaka mwili kupelekwa Kanisa la Kipentekoste la Ufufuo na Uzima ili aombewe ili afufuke, huku ndugu upande wa baba mzazi ukitaka taratibu za maziko ziendelee kwa imani ya Kikatoliki na mwili usafirishwe kwenda Moshi kwa maziko au mchungaji afike nyumbani kwa maombi hayo wanayoamini ya ufufuo.
View attachment 3207773
Huyo mama amegoma mwanawe kuzikwa anataka afufuliwe! Baba ya matehemu anataka mwanawe azikwe.
Unapoandika usipotoshe.
 
Mungu katuumba na akili na utashi kusudi tuweze kukabiliana na changamato tunazokutana nayo.

Unajua kabisa haya ni Malaria na dawa zake unazijua na pesa mfukoni unazo hutaki kutumia unataka kuombewa. Kama sio kumjaribu Mungu wako ni nini?
Umeonae! Yaani ilifika hatua mme wa huyo mama na mama mkwe wake wakatibuana sababu ya misimamo tofauti. Mama mtu anang'ang'ana bintie akaombewe kwa Mwamposa, lakini mme mtu anahitaji mke wake atibiwe hospital. Ila trials zote zilifanyika, mme mtu kaibuka mshindi, kwasababu kwa Mwwmposa hakuambulia chochote zaidi ya kuambiwa labda hakuwa na imani.
 
Waombezi matapeli, lengo lao ni pesa za hao waumini waliogeuka matahira !
 
Back
Top Bottom