JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia mmoja wa wafungwa ambao waliachiwa huru kwa msamaha wa Rais mnamo Mei Mosi, 2022, Nestory Elias (62) kwa tuhuma za mauaji.
Elias anadaiwa kumuua Mwajuma Sadru (75), Mkazi wa Mtaa wa Bong'ola kutokana na mgogoro wa kugombania eneo la biashara ambalo mtuhumiwa alikuwa akilitumia kwa ajili ya biashara ya kuchoma mihogo.
Marehemu alimtaka Elias aondoke eneo hilo, mtuhumiwa akamtishia kumuua Mwajuma ambaye alienda kutoa taarifa Serikali za Mtaa, wakati viongozi wakijiandaa kushughulikia tukio hilo ndipo Elias akafanya mauaji hayo.
Chanzo: Azam TV