Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia mpigadebe wa mabasi ya Abood Abdilah Yassin (32) mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kumuua mpiga debe mwenzake wakati wakigombea abiria kwenye stendi kuu ya mabasi Msamvu.
---
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Abdilah Yassin mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro mpigadebe wa basi la Abood katika kituo kikuu cha mabasi cha Msamvu mkoani Morogoro kwa kusababisha mauaji kwa kumchoma kisu mpigadebe mwenzie wa basi la BM Tazani Mndeme mkazi wa Mwembesongo wakigombea abiria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Machi 28 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi katika stendi hiyo.
Amesema katika ugomvi huo wa kugombea abiria Abdilah Yassin ambaye anafahamika zaidi kwa jina la "HAJIMONGA BONGE" alimchoma kisu kifuani upande wa kushoto Tazani Mndeme ambapo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na kufariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.
Source: WasafiDigital