Morogoro: Mpiga debe amuua mpiga debe mwenzake wakigombea abiria stendi ya Msamvu

Morogoro: Mpiga debe amuua mpiga debe mwenzake wakigombea abiria stendi ya Msamvu

Shangaa wewe, eti mtu umetoka zako nyumban unaenda kupanda gari ya kwenda mwanza afu kuna mtu anatokea hapo katikati anaseema amekuleta!
Kama magari ni mengi ya kwenda mwanza na huna tiketi mpiga debe yuko sahihi anakuwa amekupeleka kwenye hilo gari A sababu pengine bila yeye ungeweza kwenda gari B na kumbuka sio abiria wote wanaufahamu wa magari ya huko anakoenda.

Ila siungi mkono wapiga debe.
 
Vijana wanaotafuta abiria Kwenye mabasi wameuwana leo asubuhi stand ya msamvu kisa kugombea abiria maarufu salange.
 
Bangi imemtuma vibaya. RIP Mtanzania mwenzetu
 
Kama magari ni mengi ya kwenda mwanza na huna tiketi mpiga debe yuko sahihi anakuwa amekupeleka kwenye hilo gari A sababu pengine bila yeye ungeweza kwenda gari B na kumbuka sio abiria wote wanaufahamu wa magari ya huko anakoenda.

Ila siungi mkono wapiga debe.
Wasimamizi wa stand wakiweka utaratibu mzuri inawezekana kabisa, wenzet Rwanda tu hapo wanaweza, kumbuka wapiga debe wanawashika hata abiria wanaosafiri na kampuni yenye mabasi mengi mfano Abood, BM
 
Mimi nilikuwa ni mmoja ya watu nnaochukia sana hawa watu the way ukifika stand wanakupigia makelele kila mtu anakuuliza unapoenda na anataja gari lake.

Siku hiyo nilikutana na jamaa nkamwambia gari nnayotaka kupanda naijua na ofisi naijua so bro we pumzika usijali. Yule jamaa akanieleza tu ukweli akasema "bro samahani najua unapajua ila naomba tu twende wote ili ionekane nimekupeleka sababu namimi napata kitu nikikupeleka". Wengi wanaopambana stand ni vijana wenzetu hivyo tusiwachukie.

Mwisho ukienda stand we tafuta mtu mmoja then muelekeze unachokitaka.
Lastly, R.I.P kwa mtanzania mwenzetu
 
Tatizo hapo sio wapiga debe bali ni polisi na wamiliki wa mabasi!! Inakuwaje mtu utoke kwako ushapanga safari yako kisha ufike stendi ya mabasi uanze kugombaniwa kama mpira!!? Kuna haja gani ya kujenga stendi kwa mabilioni ya pesa huku la wapiga debe likiendelea tu kuachwa kama lilivyo!!? Hakuna utaratibu mzuri kabisa kwa usalama wa abiria na mizigo yake,. Naona siku hizi hadi wapiga debe wa lodge nao wameanza kuwa usumbufu yaani abiria akishuka tu tayari wanamdaka na kumsonga songa ili akalale kwenye lodge zao na tatizo hapa ni utaratibu wanaoutumia wa kumvuta abiria/mteja kisa eti wamemuwahi!! Yaani unakosa chaguo lako kisa kuna mpiga debe kakuwahi so ni lazima upate huduma yake hata kama haina kiwango!!?
 
Back
Top Bottom