Nyetk
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,648
- 1,698
Hao wenzetu hawakusubiri tu halafu wakajikuta wameyafikia hayo maendeleo. Maendeleo pamoja na mambo mengine ni transformation, yaani kubadilisha fikra zetu na namna ya kutazama mambo, na siyo kukaa tu na kusubiri maendeleo yaje. Daima ni jukumu la raia kubadili mtazamo wa watawala na siyo watawala kubadilisha mtazamo wa raia. Vinginevyo watawala watapenda daima status quo maana ndiyo inayolinda masilahi yao.Kweli kabisa.hatujafikia hapo jamani ndio maana kuna kautamaduni pia ndani ya maisha yetu.huko juu wamefikia hapo kwenye "freedom of speech" wakisaidiwa na utamaduni..sasa kwa jamii zetu ambapo mamamkwe hatakiwi aone hata sura ya kidume aliyeoa mwane haya maneno yangeachwa kwanza tusogeesogee hata 2050 huko ili kizazi hiki kipite..shule za kata zimeleta uchangamfu kiasi kwamba yale yaliyokuwa yakitokea Dar enzi hizo yalikuwa yanafika bara baada ya mwaka mzima.misemo,fasheni n.k.lakini kwa hivi sasa jambo la hovyo likitokea Dar linasambaa ndani ya nusu saa hadi kwetu ihanzutwa kule mafinga. Huko kwenye freedom of speech wanaruhusu ndoa za jinsia moja,wasagaji n.k.....Ni sawa lakini nadhani bado tunahitaji kulinda na kuheshimu mila na utamaduni wetu wa kuheshimu wakubwa zetu na kutowatolea maneno ya kejeli kupita kiasi.
Kinachokatisha tamaa hapa kwetu bado tunadhani watawala wana haki ya kulinda hali ibaki hivi hivi ili waendelee kupiga maisha tukidhani ifikapo 2050 kutakucha tu tujikute maendeleo yako mlangoni. Hiyo ni kujinyonga wenyewe na kamwe mabadiliko hayatakuja kwa mtindo huo. Ee Mungu tusaidie watz tujitambue.