Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Wasanii na sanaa ni kioo cha jamii kwamaana kwamba inachokifanya jamii kioo kitaonesha na kioo hakidanganyi iweje ukatae kioo kikikuambia ulivyo uanze kubishana nacho . Badala ya kujirekebisha

[HASHTAG]#kioo[/HASHTAG] hakidanganyi#
 
Issue siyo kumuiga Mange. Watanzania wemechoka uonevu. Kwa mwendo huu natabiri Tanzania kuzalisha wakimbizi kwa maelefu kabla 2020.
uonevu gani wewe ulioupata? ndugu eleza uonevu wako na sio kuegemea kwa wengine
 
Yesu alimaliza kazi yake ndipo akasurubiwa lakini mbegu ya neno ilikuwa ishapandwa kwenye mioyo ya wanadamu..

Ney kasha fanya kazi...
Kumkamata nikusaidia tu wimbo uwafikie watu wengi zaidi,wengi watataka kujua ameimbaje hata kumpelekea akamatwe?; kwa hivyo serkali inajitshidi kujinyoga yenyewe
Nadhani serikali ijikite kwenye kutekeleza yaliyomo kwenye ilani yaliyosababisha wananchi wakaichagua CCM, haya mengine yatawapotezea muda bure, maana waliokuwa wakizunguusha mikono kwenye kampeni walikuwa wengi sana hakuna mahabusu zitakazowatosha hata kama ungependa kuwatia ndani wote. Tuangalie picha kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi kuelekea 2020 na kuendelea, hivi vidogovidogo vitaichelewesha serikali bure katika kutimiza yale iliyowaahidi wananchi.
 
Nakuelewa unachosema mkuu. Tatizo labda reference yako ni Tz yetu ya Magufuli. Ungetembea kidogo huko duniani ungelewa ninachomaanisha. Kwa wenzetu walioendelea wimbo kama huo itakuwa ni kichekesho mtu kukamatwa.
Kweli kabisa.hatujafikia hapo jamani ndio maana kuna kautamaduni pia ndani ya maisha yetu.huko juu wamefikia hapo kwenye "freedom of speech" wakisaidiwa na utamaduni..sasa kwa jamii zetu ambapo mamamkwe hatakiwi aone hata sura ya kidume aliyeoa mwane haya maneno yangeachwa kwanza tusogeesogee hata 2050 huko ili kizazi hiki kipite..shule za kata zimeleta uchangamfu kiasi kwamba yale yaliyokuwa yakitokea Dar enzi hizo yalikuwa yanafika bara baada ya mwaka mzima.misemo,fasheni n.k.lakini kwa hivi sasa jambo la hovyo likitokea Dar linasambaa ndani ya nusu saa hadi kwetu ihanzutwa kule mafinga. Huko kwenye freedom of speech wanaruhusu ndoa za jinsia moja,wasagaji n.k.....Ni sawa lakini nadhani bado tunahitaji kulinda na kuheshimu mila na utamaduni wetu wa kuheshimu wakubwa zetu na kutowatolea maneno ya kejeli kupita kiasi.
 
Nadhani serikali ijikite kwenye kutekeleza yaliyomo kwenye ilani yaliyosababisha wananchi wakaichagua CCM, haya mengine yatawapotezea muda bure, maana waliokuwa wakizunguusha mikono kwenye kampeni walikuwa wengi sana hakuna mahabusu zitakazowatosha hata kama ungependa kuwatia ndani wote.
Wananyakua tu viherehere
 
hajamtaja mtu. kama mtu anahis katajwa ajitokeze. ujue mbele ya koti unahitaj wereji wa juuu kumshtk mtu
 
Back
Top Bottom