Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Weshaona fashion sikuizi kutukana, wameharibu jf sikuhizi nayo hovyo tu, huyo wanayemuiga yuko States na hawezi kanyaga Tz, muda si mrefu jf tunaipoteza maana naona hata mods ni kama wanatumika.
Umetumwa kuingia huku?si ushinde Facebook huko.
 
sababu nini??
amishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.

[http://dashboard]

Kama Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.

Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.
 
kama hayo maneno ulio malizia ndiyo yapo kwenye huo wimbo basi anastahiri kukamatwa bila hata ya basata kuhusika na kama wewe ndiye uliye andika basi unastahiri kuwa sero mda huu huwezi kukosoa mtu au kitu kwa kutenda kosa .

Uoga ndio ulimuua mtu mjinga
 
KESI YA UCHOCHEZI YA NEY WA MITEGO NA WIMBO WAKE MPYA WAPO
NA
,Mdude nyagali
WAKILI; unasema wewe ni afisa wa polisi ney wa mitego alifanya uchochezi kwenye nyimbo yake na baadhi ya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka yameandikwa kichaa kapewa rungu hebu iambie mahakama kichaa aliyemsema ney ni yupi?
SHAHIDI PC;;kichaa aliyemsema ney ni mtukufu
WAKILI;;ifafanulie vizuri mahakama wewe ulijuaje kama kichaa aliyeimbwa na ney ni mtukufu?
SHAHIDI PC.;mimi nilihisi kuwa atakuwa mtukufu kwa kuwa ney ni timu ukawa;
WAKILI;;shahidi hivi unafahamu kuwa ushahidi wa kuhisi na kupiga ramli mahakamani haupo kwa kuwa sio kwa mganga wa kienyeji na haupo kwenye sheria yoyote?
SHAHIDI PC;;ndiyo
WAKILI;;Sasa ebu iambie mahakama bila kuhisi huyu kichaa kapewa rungu aliyemuimba ney ulijuaje ni mtukufu?
SHAHIDI PC;;kimya
WAKILI;kuna maneno mengine unayakumbuka ambayo ni ya kichochezi na yapo kwenye wimbo wa ney?
SHAHIDI PC;ndiyo
WAKILI;;unaweza kuyataja?
SHAHIDI PC;;1,kuna watu hawana malinda,,2.daudi bashite kavoji vyeti,,,3.hutaki ushauri unajifanya ndugu yake yesu
WAKILI;kwa hiyo watu kutokuwa na malinda ni uchochezi?
SHAHIDI PC;ndiyo
WAKILI;ebu iambie mahakama nini maana ya kutokuwa na malinda?
SHAHIDI PC;;kimya
WAKILI ;;jibu mheshimiwa HAKIMU anasubili a note jibu lako
SHAHIDI;;sijui ila nilisikia bungeni mbunge wa mbeya mjini mheshimiwa mbilinyi akiongea kuwa gavana akaguliwe malinda.
WAKILI ;je wewe una hiyo malinda?
SHAHIDI PC;sina na siijui
WAKILI;;Kwa upelezi wako kama afisa wa polisi ulijua ney wa mitego anamsema nani ambaye hana malinda?
SHAHIDI PC;katika kufanya upelelezi tukishilikiana na ofisi ya OCCID na ofisi ya RCO tuligundua ney alikuwa anamsema gavana wa mkoa wetu kuwa ndiye hana malinda
WAKILI;wewe ulijuaje kama ney anamsema gavana huenda alikuwa anakusema wewe na wewe si umesema hapa na mahakama ime note kuwa huna malinda?
SHAHIDI PC;hapana sio mimi ni gavana
WAKILI;;;Kwani kuna mstari wowote wa huo wimbo gavana ametajwa?
SHAHIDI PC;;hapana ila ametajwa kwa jina la daudi bashite;
WAKILI;;;kwani gavana alishawahi kusibitisha popote au kanisani ama kiapo cha mahakama kuwa jina la daudi bashite ni lake?
SHAHIDI PC;;sijui ila naona kwenye mitandao watu wanamuita hivyo.
WAKILI;;huko kwenye mitandao ni akina nani wanamuita hivyo?
SHAHIDI PC;akina Mdude Chadema Nyagali, Malisa GJ, Daniel Ezekiel Daniel Kumbusho Dawson Kagine Michael Mwaikenda Boniface Mwabukusi Yericko Nyerere Bob Chacha Wangwe Boniface Jacob Julius S. Mtatiro mange kimambi Tanzagiza Hilda Newton Chadema Karama Kaila na wengine wengi
WAKILI;;je unaweza kumleta gavana ili aje aisibitishie mahakama kuwa yeye ndiye bashite halafu ndio tuendelee na tafsiri ya neno malinda?
SHAHIDI PC.;itakuwa ngumu mheshimiwa kumleta gavana.
WAKILI;;unafahabu kwa mujibu wa sheria usipo mleta gavana kuthibitisha kuwa yeye ndiye daudi bashite ushahidi wako kuhusiana na malinda unakosa uhalali mbele ya mahakama tukufu?
SHAHIDI PC;kimyaaa
WAKILI;unafahamu kuwa kwa mujibu wa katiba serikali yetu haina dini ila wananchi wake ndio wana dini?
SHAHIDI PC;;ndiyo
WAKILI;;unakubaliana na mimi kuwa kwa mwongozo huo wa katiba ili uwe na undugu na yesu ni lazima uwe myahudi au muisrael?
SHAHIDI;;Ndiyo
WAKILI ;;sasa haya maneno unayosema ni ya uchochezi kwenye wimbo wake kuwa hashauliki ana undugu na yesu ulijua ney anamsema ni nani?
SHAHIDI;;ney alikuwa anamsema ni mtukufu kwa kuwa wapinzani hulalamika kuwa mtukufu hashauriki.
WAKILI;;kwani mtukufu ni muyahudi?au ana vitambulisho vyovyote vinavyoonyesha ni muisrael ama viashilia vinavyoonyesha ana undugu na yesu?
SHAHIDI;;kimyaaa
NINGEKUWA WAKILI MIMI MDUDE HAKIKA KESI YA NEY NINGEJITOLEA KUISIMAMIA BURE.
Mdude nyagali
sumu ya nyigu
 
Kama alifikiri ana uhuru not to that extent,wachitiii
 
Nilijua ni live mubashara!!!

Ai wishi ai kudu be
 
Hakuna kesi hapo hakuna kesi,labda wamcheleweshee dhamana tu
 
Wamemdaka! Ndiyo,ni huko Morogoro.
Msanii Ney wa mitego amekamatwa na Jeshi la polisi.Chanzo cha kukamatwa kwake hakijawekwa wazi hadi sasa.

Lkn wabashili wa mambo wanahusisha kukamatwa kwake na wimbo alioutoa hivi karibu ugusao moja kwa moja na mambo ya siasa.

Picha linaendelea.
 
Hahahahaaa wamesikia wahusika kumbe....aaaa we mtu gani hutaki kushauriwa...unajikuta unaundug na Yesu eeeeeh
 
Nakuheshimu sana naomba nisikujibu maana na we nowadays ni walewale tu..
Hamna kaka



nay yy kaimba tu je kamtukana nanii hapo kuna jina la mtu hapo kwan tanzania kuna mtuu anae itwa bashite

[HASHTAG]#bashite[/HASHTAG] mwenyewe si amelikataa jina lake au yy atuliee tuuuuuuuu
 
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.


Kamanda Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.


Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…