Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Hayo maneno ya mwishoni kamtukana nani na kwa ku semaje.
Aibu br...pakua huo mziki utausikia.lengo ni jema ila contents na ukali wa maneno kwakweli unaleta ukakasi kidogo na hasa pale anaposema watu wamemkumbuka kikwete maanake anaonesha ni nani amemtageti na hayo matusi...sio sawa ktk nchi yenye watu wenye tamaduni ambazo bado zinaheshimu wakubwa.huko kwa wenzetu wala haina shida.sisi hatujafika huko
 
Wenye heshima wataheshimiwa, sio lazima kuwaheshimu wakoloni* heshima hailazimishwi.
 
hapa nausikiliza inawezeka aliyetoa amri ya kukamatwa kwake ni huyo aliyepoteza marinda
 
Hv unazan hvyo viwanda utavipata kwelii au utaambulia viwonder tuu
Yaan wakuluu wako chonjo kuangalia ni nani anaempinga na kusoma mitandao inasemajee ila poa freedom will come soon
Ila hyo kesi lissu ataisimamia na hakuna mtu atakaefungwa hapa
 
Hapa watanzania ndo tutaelewa kwanini awamu ya nne waliogopa kutaja majina ya wauza madawa.
Yote yanayotokea mpaka hapa chanzo ni pale kwenye madawa.
Mpaka sasa watu wanaungana kila kukicha wakimshambulia yule aliyeanzisha vita ya madawa ya kulevya lakini mwanzo hatukuona wakiungana kwa nguvu kama hizi kupinga madawa ya kulevya.
Tunadai tunauchungu na nchi yetu, kwa sababu Rais katunyima Uhuru, mbabe, anavunja sheria, hashauriki n.k.
Lakini je mbona hatukuwa na uchungu kwa mania ya vijana wanaokuwa mateja wa unga kila kukicha??
Inamaana lisingekuwepo suala la madawa tusingejua habari za bashite na kama ni hivyo basi tujue hapa tunapumbazwa ili tuondoke kwenye lengo husika yameanzishwa mambo ya kutugawa ili tusisimame kwenye lengo moja la kupinga madawa na kwa hili naona wamefanikiwa kwa kiasi fulani.
Inasikitisha sana kuona watanzania tumezidiwa akili kwa kipindi kifupi sana.
 
wale wanaogomea front page, waliopoteza marinda, walofoji vyeti na maamuzi ya kisen*e ndo wamenuna kusikia huu wimbo!
 
Hv unazan hvyo viwanda utavipata kwelii au utaambulia viwonder tuu
Yaan wakuluu wako chonjo kuangalia ni nani anaempinga na kusoma mitandao inasemajee ila poa freedom will come soon
Ila hyo kesi lissu ataisimamia na hakuna mtu atakaefungwa hapa
Wanatudisha harakati za chadema nyuma kwa mambo ya kijinga
 
Uhuru wako ukiutumia vibaya ujue unajigharim mwenyewe.

Nani alikupa Uhuru wa kutukana? Hata Mwenyezi Mungu mwenyewe hakuruhusu kila kitu ujifanyie unavyotaka bana.

Hakuna Uhuru wa kutukana,kukejeri,na kutumia lugha ya maudhi.
Mmebaki na mihemko ametukana hamna hata mmoja wenu aliyetaja hilo tusi.. Na wewe umekuja na yale yale taja tusi.. Zaid ni kufata mkumbo
 
Heshima ya mtu haitokani na umri, kazi au cheo chake ndani ya jamii, bali huduma yake kwa anaowahudumia (Nyerere). Aina ya huduma na unavyoitoa ni muhimu sana kwenye upataji wa heshima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…