Hii serkali bado haijatambua kosa kubwa inalolifanya la kuwafanya watu kuonekana mashujaa (heros ) au kuwataftia kiki.
Kwa mfano, hivi sasa ni ukweli usiopingika kuwa ushindi wa kishindo wa Lissu ilibustiwa na ile hali ya kuwekewa vikwazo na serkal.
Nape leo anaonekana shujaa tu baada ya kuoneshewa bustola na askari aliyetumwa kumzuia asiongee na waandishi wa habari.
Leo lema naye hivyo hivyo. Anaonekana kama mandela wa Tanzania, baada yakufanyiwa figisufigisu za kumuweka gerezani takriban miez mitano.
Jana Mange kimambe kaweza fikisha one million followers sababu ya kupata umaarufu baada yà kushikilia kidedea vyeti vya Makonda. Yani hivi sasa followers wa mange wanaongezeka kwa 2k followers kwa siku huku followers wa makonda wakipungua kwa kasi.
Leo sasa Ney wa mitego inasemekana Tyar yupo mikononi mwa Polisi. Na sababu hasa itakuwa ni wimbo alioutoa juzi. ( jina sijafahamu unaitwaje ila kuna sehemu wanaitikia " wapo")
Siku ya leo habari za Ney kukamatwa zinaenea mitandaoni na vyombo vya habari vyote. Kesho ni front page magazetini. Na kila atakayepata hii habari lazima autafte huu wimbo ausikilize ili ajue Mantic ya uo wimbo kupelekea kukamatwa kwa Ney.
Kuja kufika kesho. Huu wimbo utakuwa ukipigwa kila mtaa. Hata wa kule kijijini kolomije mpka sasa watakuwa wamesha upata.
Serikali ingekaa kimya na kuupuuza huu wimbo basi hata wanaousikiliza wangeupuuza. Sasa kitakachotokea hivi sasa ni kila mtu atausikiliza ili ahoji ni kwa nini Ney akamatwe?
Nakumbuka kuna kipindi Nikk mbishi alitoa wimbo akimsifu kikwete. Cjui basata au TCRA wakamuita na kuufungia. Mi binafsi nilikuwa sijausikiliza maana si fani wake. Ila niliutafta nikausikiliza ili nijue kilichoimbwa mpaka ukafungiwa.
Katika hii dunia ya Utandawazi na Technology. Serikali inajisumbua kucontrol kila kitu wanachotaka wananchi wao wasikie au waambiwe. Yani hapa serkal IMECHEMSHA.
Walifanikiwa nini Pale walivyopiga marufuku wimbo wa Viva Roma 2015?
Serikali iconcentrate na Mambo ya kimaendeleo sio personality. VIWANDA HAVIJENGWI KWA KUMKAMATA NEY BHNA.
Kodi zetu Mnatumia ovyo hamtaki tuseme. Kama hamtaki kusemwa mstep down wapo ambao wapotyar kuongoza nchi na kukubali kukosolewa na Wananchi wao.