Endasak Masqaroda
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 1,728
- 3,958
Hawa dawa ni kupiga sumu shambani. Ng'ombe 100 wakifa hapo, wanahama wenyewe bila kelele.
Watu wamechanganyikiwa vibaya sn. Huu ni upunguani first levelMnaye mlilia yuko busy na yakeView attachment 3279770
Chawa, wapambe ndio kiini cha haya yote😭😭😭Watu wamechanganyikiwa vibaya sn. Huu ni upunguani first level
Matatizo haya yanasababishwa na Serikali kwani hawatilii maanani matatizo ya wakulima. Mfugaji hana shida, ikiwa ana njaa atauza ng'ombe anunue chakula, je mkulima anayetegemea shamba lake, atakula nini ikiwa mazao yake yanaliwa na mifugo huku serikali ikikaa kimya? Suluhisho hapa seiikali isiruhusu mfugaji yoyote kuishi karibu na mashamba ya watu na kama mfugaji akionkekana akamatwe mara moja na kutiwa ndani ili iwe fundisho kwa wafugaji wengine. Mapori yapo mengi sana hapa Tanzania, tunawaendekeza wafugaji ili iweje?Mkazi wa Kijiji cha Lubungo Kata ya Mikese wilayani Morogoro Mzee Yahaya Yahaya, anayekadiriwa kuwa na Umri wa Miaka 70 hadi 80, ameuawa kwa kucharangwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa ni Wafugaji, wakati akijaribu kuwazuia wasiingize Mifugo shambani kwake, hali iliyosababisha wananchi kugomea kuzika mwili wake hadi watakapopata suluhu ya serikali, kuhusu malalamiko yao dhidi ya changamoto za aina hiyo katika maeneo yao.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Lubungo anakiri uwepo wa mfululizo wa matukio ya Wafugaji kuvamia mashamba ya Wakulima, lakini baadhi yao hufanikiwa kupata haki zao baada ya tathmini.
Lakini Lisu alimuita dikteta uchwara😎Magufuli alikomesha
Ndo wanavyofanya hawa watu, wanakera mno. AaahAta bukoba maeneo ya bubale kulikuwa na wafugaji kutoka Uganda 'abanyankore/abaima' yaani walikuwa na kiburi. Analisha mifugo yake kwenye shamba lako ukikaa vibaya unapewa na kipigo. Ukimpeleka ofisini za kata anaonga, mkulima unatoka patupu.