Morogoro: Mzee Yahaya auawa kwa kucharangwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa ni 'Wafugaji'

Kama umeshawahi changanyikana na jamii za wafugaji utaelewa. Wale watu huwa ni wakorofi sana,siyo wamasai wala wasukuma,na bahati mbaya huwa wanawazidi wakulima kipato,ataharibu shamba atakupiga ukashtaki atahonga na kutoka na kuendelea na maisha kama kawaida,ikiwezekana na wewe anakulipa fidia. Wanakiburi sana hata mwenyekiti wa kijiji au mgambo hawezi wakamata peke yake zaidi ya polisi. Nishashuhudia eneo X kuna mtaalamu aliwaona wanahamisha ng'ombe eneo moja kwenda jingine m,jambo ambalo linahitaji kibali-wakamgomea na kulikuwa na mgambo karibu. Kumuuliza kwanini usimwambie mgambo awazuie? Akasema watampiga vibaya,na huwa hawatembei bila pesa isiyo na matumizi
 
Matatizo haya yanasababishwa na Serikali kwani hawatilii maanani matatizo ya wakulima. Mfugaji hana shida, ikiwa ana njaa atauza ng'ombe anunue chakula, je mkulima anayetegemea shamba lake, atakula nini ikiwa mazao yake yanaliwa na mifugo huku serikali ikikaa kimya? Suluhisho hapa seiikali isiruhusu mfugaji yoyote kuishi karibu na mashamba ya watu na kama mfugaji akionkekana akamatwe mara moja na kutiwa ndani ili iwe fundisho kwa wafugaji wengine. Mapori yapo mengi sana hapa Tanzania, tunawaendekeza wafugaji ili iweje?
 
Ata bukoba maeneo ya bubale kulikuwa na wafugaji kutoka Uganda 'abanyankore/abaima' yaani walikuwa na kiburi. Analisha mifugo yake kwenye shamba lako ukikaa vibaya unapewa na kipigo. Ukimpeleka ofisini za kata anaonga, mkulima unatoka patupu.
Ndo wanavyofanya hawa watu, wanakera mno. Aaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…