Ni mkoa mzuri sana na wenye vipaji lukuki lakini naungana na
MINOCYCLINE hapo juu kwa hoja alizotoa maana ni ukweli mtupu,japokuwa vipaji ni kweli vipo aisee maana tukiangalia nyanja hizi tunapata jibu...
1.Kisoka...
Ukiachana na timu za Dar Morogoro inafuatia kuwa na timu nyingu zilizowahi kutwaa taji la ligi kuu nazo ni Mtibwa Sugar na Mseto ukiachana na Tukuyu stars ya Mbeya hakuna mkoa uliowah kufanya hivyo hapa Tz..na kuna timu ilikuwa inaitwa reli "kiboko ya vigogo" Simba na Yanga zilikuwa hazitoki zikicheza na timu hii
Morogoro ni nyumba ya vipaji vya soka tangu zamani Kina Mohamed Msomali,Malota Soma,Zamoyoni Mogella,Charles Boniface Mkwasa(alilelewa na dada yake mtaa wa karume Morogoro tangu akiwa kijana mdogo) na wengineo magwiji wa zamani,kwa sasa wapo kina Mkude kibabage,Dickson Job,Aishi Manula,Kelvin wa Genk,Shomari Kapombe,Kibwana Shomari n.k
2.Ngumi
Hakuna asiyejua kwamba ukitoa Dar Moro ina ufalme wake katika ngumi Francis Cheka,Cosmas Cheka,Twaha Kiduku,Mandonga na wengine kibao wanatoka Moro
3.Muziki
Zamani watu dansi walikuwa wanalifuata Moro kutoka dar kuja kuwaona Cuban Marimba ya Salum abdallah na baadae Juma Kilaza na Moro Jazz ya Mbaraka Mwishehe,,Wasanii wa Moro kwa sasa ni Rich Mavoco,Jay Melody,Belle 9,Dayna,Conboi,Tundaman na wengineo hata Salam, Babu Tale wanatokea Moro
Mwandishi wa comment hii aliishi Moro kuanzia 1982-1993