Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kamishina wa Jeshi la Polisi anayeshughulikia kamisheni ya operesheni na mafunzo CPA, Awadhi Juma amewaondoa hofu wananchi kuwa jeshi hilo litaendelea kuhakikisha usalama, amani na utulivu vinaendelea kuimarishwa sasa, wakati na baada ya uchaguzi na kamwe hawatakuwa na muhali na mtu yeyote atakayejaribu kuharibu uchaguzi.
Kamishna Awadhi alisema hayo wakati akihitimisha mafunzo ya miezi mitatu kwa askari 1,074 juu ya uongozi mdogo wa ngazi ya Sajini taji (sajenti na staff sajenti) katika chuo cha maofisa wa Polisi Tanzania cha Kidatu, kilichopo wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akasema kwa sasa hali ya nchi ni shwari, tulivu na usalama umeendelea kutamalaki kwa sababu Jeshi hilo lipo na kwamba wataendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha hali hiyo inaendelea kuwepo sambamba na kutoa wito kwa wananchi kuwafichua watu wachache watakaojaribu kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
"Tumejipanga vizuri kwenye hili,tutashughulika na watu wa hovyo hovyo wanaodhani wanaweza kufanya vinginevyo, blabla (maneno maneno) mnazozisikia zisiwanyime usingizi,uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu mkubwa" alisema kiongozi huyo mwenye dhamana ya operesheni na mafunzo kwa Jeshi la Polisi.
Chanzo: Nipashe