Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Je serikali inafahamu Mungu wa Afande selemani alipo?
 
tena anapaswa atiwe adabu ili aache kabisa kuvuta bangi

dawa yake awekwe gerezani na asipate dhamana miaka 3 hapo nadhani akitoka baada ya miaka 3 atajifunza adabu na heshima.

yaaani amefika mahala akadhani hapa duniani yuko peke yake.
atiwe adabu.

ashughulikiwe ipasavyo.
 
Tatizo sio kuamini. Mungu.
BALI KUMTUKANA.
Swali kwanini UMTUKANE?
unajua mbingu na ardhi ni MALI YA NANI?
Hivi unajua duniani kuna mamilioni ya watu ambao hawaamini kuwa kuna Mungu na Mungu hata siku moja hajawahi kuwaadhibu? Kwa nini mnataka kumfundisha Mungu kazi?
 
aina ya watu kama huyu mvuta mibangi ndio wakiachiliwa na tabia kama hizi ndio wanao sababisha laaana na majanga ktk Taifa, ashughulikiwe ipasavyo.
atupwe gerezani na asipewe dhamana miaka 3 inamtosha.
 
Kwenye sala ya Baba Yetu (RC) kuna msitari unasema, "Tusamehe dhambi zetu kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea".
Unaweza ukasamehewa kiroho, lakini Jamhuri lazima ikuchukulie hatua. Kwani watoto wa shule wakipewa ujauzito na familia zikasameheana, Serikali ikijua itamuacha mtuhumiwa?
 
Katumia lugha ya matusi kupost kwenye mitandao kitu ambacho kinaangukia kwenye Cyber crime law.
 
Tokea lini Serikali imekuwa na Dini?
Polisi wa Tanzania wana vituko! Nani amewapelekea malalamiko? Au wameanza fanyia kazi RB za mitandaoni? Yeye imani yake imemwaminisha Mungu hayupo, unataka kumlazimisha akili imani muitakayo? Badirikeni, muda si rafiki kwenu.
 
Unaweza ukasamehewa kiroho, lakini Jamhuri lazima ikuchukulie hatua. Kwani watoto wa shule wakipewa ujauzito na familia zikasameheana, Serikali ikijua itamuacha mtuhumiwa?

Afande Sele kaikosea serikali kwa misingi ipi?
 
Naomba asamehewe, nadhani ni kitete cha majonzi kilimshika mpaka mdomo ukakosa busara na lijamu! asamehewe jamani!
 
Kama haina dini basi iruhusu watu kukashifu imani ya wengine?
Kuna watu wanaamini Mungu hayupo, kuna watu wanaamini Mungu yupo. Nani ana mkashifu mwingine? Suruhisho: kila mtu ashikilie imani yake, serikali ishughulike na yule amnyoosheae kidole mwenzake.
 
Sisi kama jeshi la polisi tunamhoji mhusika kuhusu bangi alizozitaja. Hilo la Mungu bado hatuna ushahid wa kutosha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Very very good idea. Hoja ya Mungu wala polisi haiwahusu, ukitafuta ushahidi, utamaliza vitabu vya duniani.
 
Jamani Mbona mnampa misukosuko ?!

Muacheni Mungu mwenyewe anahuruma na kusamehe .
 
Back
Top Bottom