Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Msameheni tu maana hajui alitendalo ,hata yule shehe ubwabwa aliyesema afe sijui ndani ya siku saba sio kazi yake na wala yeye sio Mungu ndiomaana dua zote ama laana zote wanasema Mungu aone cha kumfanya sio yeye aamrishe eti afe kabla ya Ramadhan who is Kishki hekima ni kitu Muhimu sana hasa unapokua kiongozi uwe wa Dini ama Siasa
 
Kuna watu wengine tena viongozi wa dini walidiriki hata kumlinganisha magufuli na Mungu lakini mbona hao hawakukamatwa??!!
 
Msameheni tu maana hajui alitendalo ,hata yule shehe ubwabwa aliyesema afe sijui ndani ya siku saba sio kazi yake na wala yeye sio Mungu ndiomaana dua zote ama laana zote wanasema Mungu aone cha kumfanya sio yeye aamrishe eti afe kabla ya Ramadhan who is Kishki hekima ni kitu Muhimu sana hasa unapokua kiongozi uwe wa Dini ama Siasa
Hata George Bush alipigwa laana afe baada ya mwezi akaishia kupaliwa na mfupa na laana ya kutupiwa viatu.
 
Msanii mkongwe wa muziki, Selemani Msindi maarufu Afande Sele, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mjini Morogoro kwa mahojiano baada ya video yake iliyokuwa na maudhui ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai hakutenda haki kuruhusu kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli.

Hivi karibuni afande Sele alisikika akimlaumu Mungu kuruhisu Magufuli afe.

Mkuu wa Polisi Morogoro kasema kesho ataongea kinagaubaka sababu za kumkamata na kumlaza Korokoroni.

Zaidi soma: Afande Sele( Seleman Msindi), asomewa dua ya kufa kabla ya Ramadhan ya 2021 kufika, atuhumiwa kumkufuru Mungu
View attachment 1732037

Nimeisikiliza hiyo video, hajamtukana mtu awaye yeyote...

Amerusha lawama na matusi yake kwa Mungu. Na huyu Mungu wala hata hajalalamika, yeye anaendelea kusema tu kuwa;

"....Afande Sele pamoja na matusi yako kwangu, Mimi NAKUPENDA SANA, njoo kwangu nitakupa pumziko la Amani..."

Kama atafunguliwa mashtaka, kesi hii itakuwa tamu sana maana tutataka aliyetukanwa (Mungu) afike mahakamani kutoa ushahidi wake ili Afande Sele atiwe hatiani...
 
Kama haina dini basi iruhusu watu kukashifu imani ya wengine?
Umeisikiliza voice clip ya maneno ya Afande Sele kweli?

Mimi nimeisikiliza mwanzo mwisho. Hajakashfu dini wala imani ya mtu yeyote..

Yeye ana bifu na Mungu wake siyo na mtu au imani au dini ya mtu yeyote...

Ashtakiwe kwa kosa lingine labda la kwa kutumia sheria ya makosa ya kimtandao - Cyber Crime la " kutumia mtandao kurusha kashfa na matusi hadharani" lakini siyo hili la "kumtukana Mungu" maana halina ushahidi na haliwezi kuthibitika mbele ya sheria...
 
Alishaomba radhi asee,tena ameomba msamaha vizuri sana.

Amesema alipokea taarifa ya kifo cha JPM kwa mshtuko akachanganyikiwa na kuanza kuropoko.

Kama Mungu anasemehe sisi wanadamu ni wakina nani tusisamee?
Wanadamu tunatafutaga chance ya kunyooshana tu. Watu wanakuwa na stress au hasira zao, then wanatafuta pa kuzimwagia.
 
Msanii mkongwe wa muziki, Selemani Msindi maarufu Afande Sele, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mjini Morogoro kwa mahojiano baada ya video yake iliyokuwa na maudhui ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai hakutenda haki kuruhusu kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli.

Hivi karibuni afande Sele alisikika akimlaumu Mungu kuruhisu Magufuli afe.

Mkuu wa Polisi Morogoro kasema kesho ataongea kinagaubaka sababu za kumkamata na kumlaza Korokoroni.

Zaidi soma: Afande Sele( Seleman Msindi), asomewa dua ya kufa kabla ya Ramadhan ya 2021 kufika, atuhumiwa kumkufuru Mungu
View attachment 1732037
Amelaumu na kumtukana Mungu acha kuogopa kusema ukweli haikuwa lawama tu na matusi
 
Kitendo tu cha kukamatwa
Tayari kwetu ni toba kubwa
Lakini angeachwa ingelionekana sisi sote tumeunga mkono mitusi yake sele chandumu

Kama allah angeleta gharika hapa tanzania isingechagua wenye Dini na wasio na dini

Tungechapika wote
Ongera polisi ongera serikali
Sele mandumu kama ni laana imkute yeye pekee yake

Na kama msamaha basi ajuaye ni mungu mwenyewe ila sisi
tumeonesha hasira zetu kwa sele mandumu na allah atusamehe sote ...
 
Alishaomba radhi asee,tena ameomba msamaha vizuri sana.

Amesema alipokea taarifa ya kifo cha JPM kwa mshtuko akachanganyikiwa na kuanza kuropoko.

Kama Mungu anasemehe sisi wanadamu ni wakina nani tusisamee?

Kwenye sala ya Baba Yetu (RC) kuna msitari unasema, "Tusamehe dhambi zetu kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea".
 
Back
Top Bottom