Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Kwani amevunja Sheria gani ili tuwe na uelewa wa Pamoja
Swala la kuvunja au kutovunja mimi sijui. Mimi nimemjibu aliyesema kwakua kaomba msamaha basi asamehewe kwakua Mungu anasamehe.
 
Serikali na dini wapi na wapi?
Mbona huyo afande sele hajataja dini yoyote??
 
Et kwa usalama wake lakin Nongwa pia zinachangia inasemekana Hatati alipokua Morogoro aliwachongea baadhi ya wakubwa akiwemo Mmbunge......
 
Labda ahojiwe kwa kutaja "bangi" na "matusi"
Ila kuhusu issue ya "Mungu" ana haki yake,kila mtu ana haki ya kuwa na imani tofauti na wewe as long as haileti "violence" kwa wengine

Neno "Mungu" ni generic term,kwa wengine ni "Ngo'mbe"
Sasa sheikh mzima mkubwa tu anasimama na kuropoka eti kachukizwa Mungu wake kutukanwa

Yeye kama nani? Na Mungu yupi aliyetukanwa?
Ina maana watu wote wanaoamini Mungu katika imani tofauti nao wamlaumu Afande sele?

Halafu Mungu gani huyu anaagizwa kama jini
"Muue kabla ya Ramadhan na afe kifo kibaya"

Watu kama hawa ndo wanofanya baadhi ya "Dini" zionekane "Kituko"
 
Kama haina dini basi iruhusu watu kukashifu imani ya wengine?
Serikali haina dininndio maana hairuhusu mtu kukashifu imani za watu wengine, kila mtu aamini anachokitaka, kama sele anaamini ganja basi ailaumu ganja sio Mungu, Mungu hadhihakiwi!
 
Nadhan albadir tulomuombea inaanza kufanya kazi, na bado tegeni masikio mtayasikia mengi yakimfika uyu mvuta bhangi
Alishaomba radhi asee,tena ameomba msamaha vizuri sana.
Amesema alipokea taarifa ya kifo cha JPM kwa mshtuko akachanganyikiwa na kuanza kuropoko.
Kama Mungu anasemehe sisi wanadamu ni wakina nani tusisamee?
 
Afande sele kashikiliwa na polisi kwasababu ya matusi na sio kwamba kashfa yake dhidi ya mungu
 
Msanii mkongwe wa muziki, Selemani Msindi maarufu Afande Sele, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mjini Morogoro kwa mahojiano baada ya video yake iliyokuwa na maudhui ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai hakutenda haki kuruhusu kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli.

Hivi karibuni afande Sele alisikika akimlaumu Mungu kuruhisu Magufuli afe.

Mkuu wa Polisi Morogoro kasema kesho ataongea kinagaubaka sababu za kumkamata na kumlaza Korokoroni.

Zaidi soma: Afande Sele( Seleman Msindi), asomewa dua ya kufa kabla ya Ramadhan ya 2021 kufika, atuhumiwa kumkufuru Mungu
View attachment 1732037

Wamefanya vyema sana kumuhifadhi ndani kwa ajili ya usalama wake,kumbuka Sheikh amesoma kisomo ili Afande sele afe,kwahiyo inawezekana watu wabaya wakutumia mwanya huo kumdhuru.
 
Hiyo ni psychiatric sio police case, madaktari wafanye kazi yao
 
Wagalatia na wapagani wasio na haya wanajaribu kuficha makosa yake huyu kafiri kanakwamba hana hatia. Laana za Allah ziwe juu yake huyu kafiri afande chele na sio Suleiman. Kwanza hakustahili kupewa jina la Suleiman
 
Mtoa hoja ungeanddika hivi....Police yamshikiria kada wa CCM kwa kumdhihaki mwenyezi Mungu!!
 
Back
Top Bottom