Ni muhimu TRC wakatoa taarifa nini kilitokea kusababisha train ya jana usiku kutoka Dar to Dom kukwama zaidi ya masaa manne Kidete na kufika Dodoma karibia saa 8 na nusu usiku badala ya saa 4 usiku.
Shida yangu sio kwamba matatizo hayawezi kutokea ila shida ni customer care katika utoaji wa taarifa. Hii train ndio kwanza tumeanza na kesho ndio inazinduliwa rasmi ila hii limetia doa sherehe yote ya kesho.
Je, pre-commissioning haikufuatwa kama inavyotakiwa, tumekimbiza tu haraka kufanikisha malengo ya kisiasa?
TRC mambo kama haya wanatakiwa kuyatolea maelekezo ya kina. Jana train imechelewa display yao still inaonesha train arrival saa 4 na nusu hakuna kuonesha delays na kutoa matangazo taarifa kwanini kuna delays.
TRC toeni maelezo ya kina au ndio sabotage zimeanza.