Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Ukiiga kunya kwa tembo utapasuka msamba, Tanzania ilipaswa iimarishe tu treni iliyopo ya single gauge kuliko kung'ang'ana na vitu wasivyo viweza wakati bado nchi haina umeme wa uhakika.
 
Mimi sina shida na train ni nzuri sana, kuharibika pia sio ajabu, kuchelewa sio ajabu ila mashaka yananijia kwenye customer care, TRC walitakiwa usiku uleule kuelezea na kuomba radhi kuonesha kujali, kituoni tu hawakuweza kutoa taarifa kwenye display kama kuna delay hio ndio shida yangu.
Tukio limetokea mara ya kwanza na mpo salama watoa taarifa sio hao wanaondesha wao jukumu lao ni kuwatoa sehemu moja na kuwapeleka sehemu ingine wakiona ipo changamoto hawatakiwi kuendelea na safari hilo ni Bomu mkuu usione umelipanda huku likiwa na viti ndani ukiona umefika salama ni swala la kushuru sana pia...
 
Ila walitueleza kwa mbwembwe sana kuwa hile lidubwana lina power bank hata umeme ukikata bado ni shwaa na pia wakaenda mbele zaidi wakasema lile dubwana pia linaweza kutumia diseli likiona umeme hakuna sasa ngedere wameyazua mapya huko
 
Tukio limetokea mara ya kwanza na mpo salama watoa taarifa sio hao wanaondesha wao jukumu lao ni kuwatoa sehemu moja na kuwapeleka sehemu ingine wakiona ipo changamoto hawatakiwi kuendelea na safari hilo ni Bomu mkuu usione umelipanda huku likiwa na viti ndani ukiona umefika salama ni swala la kushuru sana pia...
Mimi siwalaumu wao nalaumu Admistration kwa maana customer care wao wanatakiwa kuwataarifu hata wapokeaji wa watu wao nini kimetokea kutokana na kuchelewa kufika basi lakini sisemi haya mambo hayatokei maana kikubwa ni usalama sio kufika haraka. Chukulia uko uwanja wa ndege unasubiri mgeni wako unaona kwenye display ndege inafika saa 4 halafu ndege hakuna mpaka saa 7 hapo hakuna taarifa yoyote ya delays uta panic, lakini huwa kawaida wanaandika pale kama departure delay na arrival time estimated sasa TRC walitakiwa tu kituoni kuweka taarifa basi hakuna lingine.
 
Back
Top Bottom