Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Lile wimbi la wanachama wa CHADEMA kujivua uanachama linaendelea
Siku ya leo Viongozi wa Chadema Mkoa Morogoro wilaya, Majimbo, Kata na Matawi wakiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Mlimba Suzan Kiwanga wamejivua uanachama wa CHADEMA.
Wakizungumza kwenye mkutano waliofanya na waandishi wa habari, wanachama hao walitaja sababu mbalimbali za kufanya uamuzi huo ikiwemo chama hicho kukosa muelekeo pamoja na kutoka kwenye malengo na misingi yake.
Miongoni mwa waliojivua ni Suzan Kiwanga aliyekuwa Mbunge Jimbo la Mlimba 2015- 2020, David Chiduo aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu Jimbo la Kilosa, Magreth Raphael alikuwa Mjumbe mkutano mkuu Taifa, Sheila Mluba Alikuwa Mwenyekiti BAWACHA Jimbo la Kilosa kati.