Morrison aishtaki Yanga TFF akidai kusainishwa mkataba ambao haufahamu

Morrison aishtaki Yanga TFF akidai kusainishwa mkataba ambao haufahamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kiungo mshambuliaji wa Young Africans, Bernard Morrison ameishtaki klabu hiyo TFF, akidai kutotambua mkataba mpya wa miaka 2 unaodaiwa alisaini kwa makubaliano maalum.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake, Elias Mwanjala imeanza kusikiliza kesi hiyo katika viunga vya Shirikisho hilo.

Mwanjala amesema mchezaji huyo amewasilisha ushahidi wake katika kesi hiyo ambayo uamuzi unaweza kutolewa leo Alkhamis, kutegemeana na usikilizaji wa pande zote, mashahidi na kamati kuridhishwa na ushahidi utakaowasillishwa.

Amesema Morrison amefungua kesi hiyo mwenyewe na alifika kwa ajili ya utetezi wa hoja zake huku Young Africans ikiwakilishwa na viongozi mbalimbali akiwemo mwanasheria ambaye pia ni kaimu katibu mkuu, Simon Patrick na makamu mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela.

“Sisi kazi yetu ni kusikiliza na kupitia ushahidi ambao pande zote mbili umewasilisha kwetu. Kama hautoshi, basi tutawapa muda zaidi, lakini kama tumeridhishwa tutatoa uamuzi, lakini siyo leo (jana) kwani kuna malalamiko mengi ukiachana na hayo,” amesema Mwanjala.

Amesema kuwa mbali ya kesi hiyo, kamati yake pia inasililiza malalamiko yaliyowasilishwa na Young Africans dhidi ya Simba ikiituhumu kufanya mazungumzo na Morrison kinyume na utaratibu, ikidai amekuwa akishawishiwa na mabingwa hao ajiunge nao.
 
Kiungo mshambuliaji wa Young Africans, Bernard Morrison ameishtaki klabu hiyo TFF, akidai kutotambua mkataba mpya wa miaka 2 unaodaiwa alisaini kwa makubaliano maalum

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake, Elias Mwanjala imeanza kusikiliza kesi hiyo katika viunga vya Shirikisho hilo

Mwanjala amesema mchezaji huyo amewasilisha ushahidi wake katika kesi hiyo ambayo uamuzi unaweza kutolewa leo Alkhamis, kutegemeana na usikilizaji wa pande zote, mashahidi na kamati kuridhishwa na ushahidi utakaowasillishwa.

Amesema Morrison amefungua kesi hiyo mwenyewe na alifika kwa ajili ya utetezi wa hoja zake huku Young Africans ikiwakilishwa na viongozi mbalimbali akiwemo mwanasheria ambaye pia ni kaimu katibu mkuu, Simon Patrick na makamu mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela.

“Sisi kazi yetu ni kusikiliza na kupitia ushahidi ambao pande zote mbili umewasilisha kwetu. Kama hautoshi, basi tutawapa muda zaidi, lakini kama tumeridhishwa tutatoa uamuzi, lakini siyo leo (jana) kwani kuna malalamiko mengi ukiachana na hayo,” amesema Mwanjala.

Amesema kuwa mbali ya kesi hiyo, kamati yake pia inasililiza malalamiko yaliyowasilishwa na Young Africans dhidi ya Simba ikiituhumu kufanya mazungumzo na Morrison kinyume na utaratibu, ikidai amekuwa akishawishiwa na mabingwa hao ajiunge nao.
Huenda mchezaji tajwa akili zake hazipo sawa!
 
Afu utopolo nao wanasema eti ilkua wachukue kombe km Simba asingebebwa. Kwa hali yenu kweli mngebeba kombe hvyo kweli. Lamda mbebe kombe la uji
 
Kwa taarifa tu huko tff alipoenda nasi pia tuliitwa tukaonesha documents zetu tff wakaamuru kijana aache ujinga mara moja arudi kazini na jana alikuwepo mazoezini na yupo kwenye safari ya kuwafuata biashara united kocha kampa masharti km anataka kusalia kwenye kikosi cha kwanza kijana kaomba radhi kuna wapuuzi tu wachache walikuwa wanamdanganya danganya na tarehe 12 in Shaa Allah atakuwepo bila kumsahau kapten papy kabamba nae karejea tafuteni pakutokea!
 
kutolewa leo Alkhamis, kutegemeana na usikilizaji wa pande zote, mashahidi na kamati kurid... leo ni ijumaa.... naamini umeibeba km ilivo
Huyu miss zomboko na football wapi na wapi bhana huyu habari zake za uhakika ambazo akileta nakuwa sina shaka nae ni za "tanzia" na "ajali ajali" niamini mm kijana karudi kundini ambacho watu hawakifahamu ni kwamba Yanga tulimiwahi Morrison kabla hajawa gumzo mjini hp tukaona hiki ni kifaa acha tukipe miaka 2 akadondoka sahihi fresh baadae sasa kila kona Morrison Morrison wapuuzi wa upande wakamfuata na kumpandishia dau kuliko tulilompa sisi ndio hpo sasa alipohisi kwamba alibugi kusaini Yanga yule ana mkataba wa miaka 2 tatzo ndio hilo hela kule anaitaka na huku alishasaini anabaki kujilaumu tu chinichini na wale jamaa nao kufuata utaratibu hawataki wanaleta uhuni uhuni hakuna kisichouzwa duniani pesa yako tu so km hela wanayo waje mezani mikataba mbona daily watu wanavunja tu? Wao si wanahela waje kuvunja huu hatuwezi acha hela km itakuwa nzuri!
 
Michezo hii wanafanya mbumbumbu fc waki mtumia mwandish Salehe Ally aliye onekana kwenye ile video akiwa anamhoji Morrison ndani ya Kambi ya Yanga.

Kinacho onekana Mbumbumbu fc hawajiamini sasa wanajaribu kucheza michezo ya nje ya uwanja jambo ambalo hawafahamu Yanga ni serikali kamili hakuna utakalo lifanya kuhujumu Timu ya wananchi ambao wako kila kona ya nchi lisifahamike. Mbumbumbu fc tulieni hakuna namnayoyote mtakayofanya kuzuia wakati yanga wanajambo Lao.
 
safari yanga tunawafunga ndani na nje ya uwanja mechi za simba na yanga siku zote anashinda ni yule anayeweza fitina sisi uwanjani tuko vizuri na nje ya uwanja pia tuko poa nyie angaikeni na maswala ya morison sisi tunajiandaa kuwaadhibu
 
kati yenu utopolo na simba nani mbumbumbu inakuwaje mchezaji anasaini mkataba na mdhamini hata viongozi wa klabu hawajui Morison alitakiwa aingie mkataba na yanga na sio gsm kule anaweza kusema alisaini mkataba wa kuuza magodoro na sio kucheza mpira
 
Legal doctrine
Inasema kama Kama mkataba ulio sainiwa baina ya pande mbili
Wakati wa kusainiwa upande mmoja ulikuwa haufahamu lugha iliyo tumiwa kwenye mkataba huo mkataba huo ni batili

Merisho sindiko vs sulus brothers case
Ameclaim masuala ya lugha kwani?..sipo aware na claims alizozitoa mkuu
 
kati yenu utopolo na simba nani mbumbumbu inakuwaje mchezaji anasaini mkataba na mdhamini hata viongozi wa klabu hawajui Morison alitakiwa aingie mkataba na yanga na sio gsm kule anaweza kusema alisaini mkataba wa kuuza magodoro na sio kucheza mpira
Mwanasheria wa Yanga alikuwepo
 
safari yanga tunawafunga ndani na nje ya uwanja mechi za simba na yanga siku zote anashinda ni yule anayeweza fitina sisi uwanjani tuko vizuri na nje ya uwanja pia tuko poa nyie angaikeni na maswala ya morison sisi tunajiandaa kuwaadhibu
Bado hamjatosheka tu!?
 
kati yenu utopolo na simba nani mbumbumbu inakuwaje mchezaji anasaini mkataba na mdhamini hata viongozi wa klabu hawajui Morison alitakiwa aingie mkataba na yanga na sio gsm kule anaweza kusema alisaini mkataba wa kuuza magodoro na sio kucheza mpira
Kwani mkataba haupo? Kweli wewe mbumbumbu
 
Back
Top Bottom