much know
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 11,461
- 17,183
Ndio hata wao walipewa na baba zaoMali za kukupa wamezitoa wapi? Wao walipewa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio hata wao walipewa na baba zaoMali za kukupa wamezitoa wapi? Wao walipewa?
Mimi naona ni tatizo la mtu binafsi, ila kama wewe una uhakika yapo mengi ya kugombea mali za uridhi;Ukanda huo kuna shida kubwa sana kuhusiana na suala la kugombea mali. Ni hatari Sana.
Kuna ushahidi gani? Kuwa na ugomvi sio kigezo..Huko moshi jamaa wa miaka 54 amemuua mama yake wa miaka 74 kwa sababu ya ugonvi wa mali alizoacha baba ama mume wa marehemu ambae ndio baba wa mtuhumiwa.
Marehemu aliacha mashamba, hayo ndio yameleta mgogoro hadi jamaa akaamua kumuua mama yake.
Matukio ya hovyo ya watu kuua wazazi wao kisa mali yanashamiri sana Kilimanjaro.
---
Adela Mushi (74), mkazi wa Okaseni, kata ya Uru kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa na shoka sehemu ya usoni na mwanaye, anayedai mali zilizoachwa na marehemu baba yake.
Inadaiwa kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 54, alifanya tukio hilo usiku wa Septemba 23, 2024 na kisha kutelekeza mwili wa mama yake ndani ya chumba chake alichokuwa anaishi.
Mwili wa mama huyo ulikutwa ukiwa umelazwa kifudifudi huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa mahojiano zaidi.
“Septemba 23, 2024 usiku wa saa 4, maeneo ya Uru Okaseni, mwanamke ajulikanaye kwa jina la Adela Dominick Mushi, aliuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani kisha kunyongwa kwa kutumia kipande cha kanga na mtoto wake aitwaye Nemes Dominic,” amesema Kamanda Maigwa.
Kamanda Maigwa amesema chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa , lakini wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu wakigombea mashamba na mali za marehemu.
Mwananchi
Kesi ya yule bint sijui unakumbuka mwaka jana ila aliachiwa huru nasikia ...Naye aliua mama yake kisa mali huko huko kilimanjaro .Dah miaka 74 mama yake si angemlea tu na sio kumuua kwa maana angemuachia tu mama ake then after a while vingerudi kwake vyote.