Moshi: Amuua mama yake wakigombea mali za marehemu baba yake

Hamna mtu mwenye akili timamu atakayeweza kufanya jambo kama Hilo. Kinachotokea hapo huyo mtoto alikuwa ni mtu wa hivyo ndio maana hata mama yake hakutaka kumpa hizo mali. Mbona ni akili kidogo Sana kumrubuni mama.
 
Ukanda huo kuna shida kubwa sana kuhusiana na suala la kugombea mali. Ni hatari Sana.
Mimi naona ni tatizo la mtu binafsi, ila kama wewe una uhakika yapo mengi ya kugombea mali za uridhi;
naomba uweke reference tatu za watu waliogombea mali ya uridhi tofauti na hiyo hapo
 
Kuna ushahidi gani? Kuwa na ugomvi sio kigezo..
 
Ndio maana wazungu ukifika 18 years you're ready to go, sasa huku kwetu wazazi wamezidi kuonea huruma watoto wao matokeo ndio haya. Kufuga fuga mwisho wanafuga majini. R.I.P ma'am 💔
 
Hamna logic unagombania mali na mama kweli!? Labda ingekuwa ndugu .
 
Dah miaka 74 mama yake si angemlea tu na sio kumuua kwa maana angemuachia tu mama ake then after a while vingerudi kwake vyote.
Kesi ya yule bint sijui unakumbuka mwaka jana ila aliachiwa huru nasikia ...Naye aliua mama yake kisa mali huko huko kilimanjaro .

Kiufupi pesa ina fitina sana , jaribu kwenda migodini uoe watu wanauawa bila ya huruma kisa pesa.
 
Mali ya baba ako aliye muoa Mama ako unaenda kugombea Kama mliolewa wote vile.
Vijana tujikaze Muda tunaopoteza ndio tunajipoteza Sisi. Muda umekubeba wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…