Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Wastaafu wengi wanapangiwa kuuwawa na watoto wao,sema tu ni chance inakosa matukio yangekuwa mengi zaidi
Malezi tu, mzazi wangu alipostaafu nilimshikisha kama 500K anywe bia hata miezi mitatu bila kugusa pension yake (maana tayari nilikuwa ajira kwa elimu waliyonilipia wazazi)...na ningekuwa na uwezo kipindi kile ningempa zaidi..sijawahi hata kuwaza kuhusu hela zake sana sana nikiwa freshi namtumia kidogo alipie hata maji na king'amuzi...hela wanazopata wakistaafu kwa kijana anaeza akaona nyingi ila kiukweli ni ndogo. Hapo hapo afanye biashara ambazo mara nyingi zinabuma hapo hapo ale hapo hapo ahonge na kuvimba kidogo kitaa hapo hapo alipe wasaidizi wa kazi nyumbani hapo hapo afanye house maintenance etc
 
Kama ulishawahi kuishi Kilimanjaro maeneo ya uchagani na Wilaya zake....ukitazama kwa umakini harakati za Wana jamii, haiba na mienendo ya Wana jamii waliokuzunguka na mitazamo yao juu ya maisha unagundua kuwa kuna tatizo mahali.

Katika hali ya kawaida wachaga ni watu wastaarabu, waungwana na wenye kujitoa sana ila tu wapo obsessed na upatikanaji wa mali......wazee wa kichaga waliihamishia obsession hiyo kwenye kupambana kila Kona ya nchi hii.....na matokeo yameonekana.....ni dhahiri kuwa ni moja kati ya makabila yaliyo fanikiwa sana kiuchumi na kielimu.

Hilo halina ubishi ukikanyaga tu mji wa Moshi utajua kuwa nipo kwenye mji wa watu waliopiga hatua kimaendeleo kuanzia ubora wa makazi ya watu, huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi.

Uharibifu umeanzia hapa kati kati baada ya kuzuka kizazi cha vijana wavivu wasiojituma kwenye kazi na wasio na nidhamu kwenye frdha kwa kuendekeza starehe za pombe na wanawake.

Kizazi hichi Cha watu wavivu kinachoamini katika njia ya mkato kwenye mafanikio ndio kimezusha na kuzalisha matendo yasiyokuwa ya kiungwana kibinadamu kwenye jamii za kichaga na kuipaka matope.

Haya matukio ni muendelezo wa harakati za hicho kizazi na yatakuja matukio mengine mengi mpaka pale watakapo rudi kwenye mstari kuwa mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa.
Mkuu tatizo ni roho tu Tatizo ulilo litaja lipo kwenye kila jamiii lakin mbona jamii tofauti na wao matukio siyo mengi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa polisi wetu ukute wamemuingizia sana chupa za mirinda na bia huyo binti huwa najiuliza Kwan hakunaga mbinu zingine za kugundua ushahidi wa haya matukio ukiacha hii ya kutesa
Hapo hamna hata haja ya kumtesa...maiti kafukia chini kwenye mchanga hata hajajengea.. yani mwela wakija na German Shepherd au Belgian Malinois mmoja ni dakika sifuri wanamsanukia
 
Ukiamua kua mhalifu angalau uwe na akili.

Hii njia ya kujibu 'Ameenda mkoa X' 'Ameenda nchi X' ni majibu ya zamani ambako hakukua na simu, mitandao wala miundombinu ya kueleweka.

Crime 1 on 1 utakamatwa kwa kukutwa na silaha ya tukio au mwili. How do you get rid of both? Hapo ndiyo itakutofautisha kati ya average criminal na not-average-criminal.
 
Hawezi kukuua anajua Mali zake zipo tu muda wowote.
Au Kama vipi muandalie mazingira mazuri ya maisha Kama kafeli shule mpe hata msingi wa biashara.
Ile kauli ya nenda katafute Mali zako sio nzuri.
Muite mwanao kaa nae kirafiki mwambie mwnang una mipango gani atakueleza mwisho wa siku mtafikia muafaka
sasa ukimuandikia urithi si ndio umempa uhakika kabisa.
 
Ukabila gani wakati ni kawaida mkuu. Sasa huyu kaua mamaye wa kumzaa atashindwa kuua mmewe ambaye Hana undugu naye Kama yule wa dumila kuwa huyo fala mmeshamaliza ama yule mkikuyu aliyemuua mholanzi akamuweka kwa shimo Cha choo jumlisha huyu dogo Arusha aliyeua mamaye akamchimbia kwa septic tank.
Sema unataka uonekane wako watakatifu Sana .
Yaani ndugu yangu akioa Kilimanjaro nitapambana Sana mpaka asioe yaani nitatishia mpaka kujiua
Dogo acha ujinga,halafu futa hii comment sababu utakuja kujitundika kweli
 
Mama alikuwa nesi???kcmc!

Matukio mengine tusiangalie upande mmoja.


Kuna vifo vingi sana vinavyosababishwa na dharau na uzembe wa ma Dr. na manesi wetu hapo tuache deal za kuuza viungo vya binadamu.


Huyu mama inawezakana kabisa kashiriki katika mauaji mengi sana huko hospitali kiasi laana imemfuata ...

Tuwe makini sana sie ambao tupo katika sehemu za kusaidia watu wemye matatizo

Makanisani,hospitalini Na kadhalika.

Matendo yetu uwaga yanahukumiwa hapa hapa dunia kama sio sisi basi kizaZi lazima kilipe.

Kwa upande mwingine vijana tuache short cut za maisha sasa hata hizo mali atazifanyia nini
Taarifa inaeleza mhusika ni mwanae. Sasa huko kwenye uwajibikaji wake inaingiaje?
 
Na kilimanjaro kwa akili yako wazawa ni wachaga tu, jiongeze acha upumbavu!! Makabila wazawa wapo zaidi matatu,,
Nimekuambia wa kuja Moshi labda ni mtumishi tu.
Mana ule mji sio rafiki kwa mgeni. Ni sawa na mkikuyu aende kwa wakalenjini atatengwaje kisa ni kyasaka.
Ivi unamjua mchagga kwa ubaguzi.yaani ukiishi kule mdanganye kuwa na wewe ni mchaga sema babu yako alipotea miaka na miaka ndo utapata favour za kutosha na wataku treat Kama wa kwao
 
Kumpa mtoto elimi ni jambo la muhimu. Zamani wakati bado tupo smal smal population hiyo elimu waa a guarantee kupata job. Mambo sasa yamebadilika kabisa.

Wasomi wapo mtaani wanahangaika....kama mtoto kaumiza kichwa na kaja na wazo zuri ambalo linahitaji usaidizi toka kwako mzazi basi ni vyema ukamsaidia.

Kama mzazi hupendi kuona mwanao anataambika...ni ule upendo wa asili wa mzazi. Hivyo basi tumia mali zako katika kumsaidia mwanao kupata mali zake.

Kama mtoto umemlea vizuri sidhani kwamba kumwambia mwanangu hizi mali zote nizochuma ni za kwetu sote hivyo nataka wewe uzitumie kuendeleza utajiri wa familia kutamfanya abweteke but rather itamfanya atambue kuwa ana jukumu kubwa na kwamba mzazi wake anamtegemea na kuthamini uwepo wake katika familia.
Unawajua watoto wa dot com, insta, Facebook unawasikia?? Hujazaa wala kukuza mkuu, ulevi ni changamoto!

Wanabweteka unawaona kabisa, wakijua ukifa watakuwepo wakitafuna jasho lako ovyo.

Kuna mahali tulikosea tulipoondoa viboko na adhabu, tukaingiza uzungu.
Wenzetu wazungu. Wanafundisha social responsibility, Ku tidy up toys, organizations kama wazazi wetu vijijini wanavyofanya, sisi mijini kila kitu dada WA kazi, mtoto katupa nguo viatu matoy dada awajibike, mtoto anapikiwa, anapakuliwa, anakula hatoi wala kuosha hata sahani yake.

Bladifakeni😕 naogopa Sana nionavyo tunavyolea watoto siku hizi, kila siku nawaambia. Mama Yao ni mke wangu wakue watafute vyao, wake zao wakuwatesa. Na wanajua kuwaona mama zao, na mama zao wanawadekeza.
Eti tuwajengee, too hell navyojenga vyangu nikimalizana kusomesha nauza kimojakimoja nakula taratibu Kwa sababu hata ukiwaachia watauza.
 
Binti mwenyewe pisi fulani anaonekana
Kwa tukio alilofanya unaweza kushangaa
Mali hizi zitawatoa roho watu

Ova
Atapata ama akipata mchumba atajilipua kuwa huyu huyu ndo wife material jamani. Rangi inavutia ile emotions zikiwa zinafanya kazi na zime overtake cortex brain hutaelewa mpaka ziishe.
Ukipata Mali tu ndo utamjua ataanza kiburi kurudi asubuhi ili uongee tu akumalize.
Kiukweli nishawahi kukuta wanawake wa kichaga wanapiga story aisee ni wakatili kinouma asikauambie.
Yaani neno nililolisikia ni "kwani huko kwao Kuna makaburi mangapi kwenye ukoo wake,je na likiongezeka la kwako Kuna hatari gani'

Ke wa kichaga weka mbali na wako smart kuwakamata watu wa kuwaoa Mana wako waerevu Sana na ukiongea naye ni suala la hela tu unajiona kuwa nimepata mke jamani hapa.kumbe mkuu unaishi jambazi ndani
 
Hii ni societal evolution. Pre-colonialism jamii za wanyamwezi, wayao walitajwa kama makabila yaliyokua kinara kwenye biashara. Leo wako wapi?
Jamii ya kichaga ilisifika kwa utafutaji mali, lakini kadri zama zinavyokwenda kizazi cha sasa si tena kama cha zamani, na mabadiliko yatakwenda mpaka itakuja tena jamii nyingine itaibuka kuwa kinara. Na itakua hivyohivyo.
 

MOSHI: BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI ILI ARITHI MALI, MWILI WAGUNDULIWA BAADA YA MWAKA MMOJA

• Meya Juma Raibu ashindwa kujizua amwaga machozi na kulaani vikali, awaasa vijana kuacha tamaa na starehe
•Meya Raibu ampongeza Rpc Kilimanjaro ACP Simon Maigwa na timu Yake Kuendelea Kusikiliza Na Kutatua Jinai Mbali Mbali


Ikiwa zimepita siku kadhaa toka litokee tukio la kijana mmoja jijini Arusha kumuua mama yake mzazi Kwa tamaa ya Mali, Limegundulika tukio lingine la kinyama mkoani Kilimanjaro katika Manispaa ya Moshi ambapo binti mmoja aliejulikana Kwa jina Moja la Wendy amemuua Mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambae ni Nesi mstaafu wa Hospital ya KCMC.

Jeshi la Polisi limeufukua Mwili huo leo tarehe 09-01-2022 katika kata ya Rau baada ya kumhoji binti huyo Kwa zaidi ya wiki mbili sasa Kisha kukiri kumchinja mama yake Kwa panga na kumfukia nyumbani hapo.

Ni takribani Mwaka sasa ndugu na majirani walipokuwa wamuulizia mama huyo walipatiwa majibu na binti huyo kuwa amesafiri Kwa matibabu nje ya nchi.

Akizingumza Kwa uchungu huku akilengwalengwa na machozi Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ndg Juma Raibu ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho na amelaani vikali tabia ya vijana kuendekeza tamaa na kukosa uvumilivu wa utafutaji Mali Kisha wanaishia kufanya matendo ya kinyama.
Namnukuu

"Kiukweli hili ni tukio la kutisha, nitoe pole Kwa familia ndugu na majirani wote mliofika hapa, nimepata huzuni sana kuona jinsi gani ya taamaa Mali imetufikisha hapa, nalaani na ninatoa wito Kwa vijana wenzangu wote nchini kuacha kupaparikia Mali na starehe mwisho wake tunageuka kuwa wanyama kiasi hiki, yaani unamuua mama mzazi?

Hivi unakuwa huoogopi laana na adhabu ya mola? nalipongeza Jeshi letu la Polisi Kwa hatua hii nawatia Moyo mwendelee na kazi hii njema ya kufichua na kudhibiti wahalifu wa namna hii na wanaoshirikiana nao".


mwisho wa kunukuu.

Tayari madaktari wameanza kufanyia uchunguzi wa postmortem Mwili huo kwajili ya hatua zinazofuata.

#MoshiBlog UpdatesView attachment 2075108

View attachment 2075109
Wachagga Mali zilishawatawala ! Endeleeni kuuana tu.
 
Back
Top Bottom