Dr Rutagwerera Sr
JF-Expert Member
- Dec 21, 2011
- 5,809
- 11,462
Dah hasara iliyoje!
Umekula hasara ulimwenguni na kesho mbele ya Mola wako.
Umekula hasara ulimwenguni na kesho mbele ya Mola wako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo Wana pigania kuchukua nchi wasimamie makusanyo yote ya nchi na maliasili za TanzaniaHawa wachaga ubinafsi umezidi Sana.
Malezi tu, mzazi wangu alipostaafu nilimshikisha kama 500K anywe bia hata miezi mitatu bila kugusa pension yake (maana tayari nilikuwa ajira kwa elimu waliyonilipia wazazi)...na ningekuwa na uwezo kipindi kile ningempa zaidi..sijawahi hata kuwaza kuhusu hela zake sana sana nikiwa freshi namtumia kidogo alipie hata maji na king'amuzi...hela wanazopata wakistaafu kwa kijana anaeza akaona nyingi ila kiukweli ni ndogo. Hapo hapo afanye biashara ambazo mara nyingi zinabuma hapo hapo ale hapo hapo ahonge na kuvimba kidogo kitaa hapo hapo alipe wasaidizi wa kazi nyumbani hapo hapo afanye house maintenance etcWastaafu wengi wanapangiwa kuuwawa na watoto wao,sema tu ni chance inakosa matukio yangekuwa mengi zaidi
Mkuu tatizo ni roho tu Tatizo ulilo litaja lipo kwenye kila jamiii lakin mbona jamii tofauti na wao matukio siyo mengi ?Kama ulishawahi kuishi Kilimanjaro maeneo ya uchagani na Wilaya zake....ukitazama kwa umakini harakati za Wana jamii, haiba na mienendo ya Wana jamii waliokuzunguka na mitazamo yao juu ya maisha unagundua kuwa kuna tatizo mahali.
Katika hali ya kawaida wachaga ni watu wastaarabu, waungwana na wenye kujitoa sana ila tu wapo obsessed na upatikanaji wa mali......wazee wa kichaga waliihamishia obsession hiyo kwenye kupambana kila Kona ya nchi hii.....na matokeo yameonekana.....ni dhahiri kuwa ni moja kati ya makabila yaliyo fanikiwa sana kiuchumi na kielimu.
Hilo halina ubishi ukikanyaga tu mji wa Moshi utajua kuwa nipo kwenye mji wa watu waliopiga hatua kimaendeleo kuanzia ubora wa makazi ya watu, huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi.
Uharibifu umeanzia hapa kati kati baada ya kuzuka kizazi cha vijana wavivu wasiojituma kwenye kazi na wasio na nidhamu kwenye frdha kwa kuendekeza starehe za pombe na wanawake.
Kizazi hichi Cha watu wavivu kinachoamini katika njia ya mkato kwenye mafanikio ndio kimezusha na kuzalisha matendo yasiyokuwa ya kiungwana kibinadamu kwenye jamii za kichaga na kuipaka matope.
Haya matukio ni muendelezo wa harakati za hicho kizazi na yatakuja matukio mengine mengi mpaka pale watakapo rudi kwenye mstari kuwa mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa.
... taarifa haijataja kabila. Na hata kama ingetaja what did you want to conclude?Kwani aliyeua siyo Mchagga?
Hapo hamna hata haja ya kumtesa...maiti kafukia chini kwenye mchanga hata hajajengea.. yani mwela wakija na German Shepherd au Belgian Malinois mmoja ni dakika sifuri wanamsanukiaHawa polisi wetu ukute wamemuingizia sana chupa za mirinda na bia huyo binti huwa najiuliza Kwan hakunaga mbinu zingine za kugundua ushahidi wa haya matukio ukiacha hii ya kutesa
sasa ukimuandikia urithi si ndio umempa uhakika kabisa.
Dogo acha ujinga,halafu futa hii comment sababu utakuja kujitundika kweliUkabila gani wakati ni kawaida mkuu. Sasa huyu kaua mamaye wa kumzaa atashindwa kuua mmewe ambaye Hana undugu naye Kama yule wa dumila kuwa huyo fala mmeshamaliza ama yule mkikuyu aliyemuua mholanzi akamuweka kwa shimo Cha choo jumlisha huyu dogo Arusha aliyeua mamaye akamchimbia kwa septic tank.
Sema unataka uonekane wako watakatifu Sana .
Yaani ndugu yangu akioa Kilimanjaro nitapambana Sana mpaka asioe yaani nitatishia mpaka kujiua
Taarifa inaeleza mhusika ni mwanae. Sasa huko kwenye uwajibikaji wake inaingiaje?Mama alikuwa nesi???kcmc!
Matukio mengine tusiangalie upande mmoja.
Kuna vifo vingi sana vinavyosababishwa na dharau na uzembe wa ma Dr. na manesi wetu hapo tuache deal za kuuza viungo vya binadamu.
Huyu mama inawezakana kabisa kashiriki katika mauaji mengi sana huko hospitali kiasi laana imemfuata ...
Tuwe makini sana sie ambao tupo katika sehemu za kusaidia watu wemye matatizo
Makanisani,hospitalini Na kadhalika.
Matendo yetu uwaga yanahukumiwa hapa hapa dunia kama sio sisi basi kizaZi lazima kilipe.
Kwa upande mwingine vijana tuache short cut za maisha sasa hata hizo mali atazifanyia nini
Moyo wa mtu kichaka, hata wewe una mengi umeyazika moyoni japo si makubwa kama haya na yanakusumbua akili unapokuwa peke yako, ni vile tu hatuwezi kuona yaliyo mioyoni mwa watu. Watu wanateseka sana katika nafsi zao kwa mizigo ya mawazo mkuu.
Nimekuambia wa kuja Moshi labda ni mtumishi tu.Na kilimanjaro kwa akili yako wazawa ni wachaga tu, jiongeze acha upumbavu!! Makabila wazawa wapo zaidi matatu,,
Unawajua watoto wa dot com, insta, Facebook unawasikia?? Hujazaa wala kukuza mkuu, ulevi ni changamoto!Kumpa mtoto elimi ni jambo la muhimu. Zamani wakati bado tupo smal smal population hiyo elimu waa a guarantee kupata job. Mambo sasa yamebadilika kabisa.
Wasomi wapo mtaani wanahangaika....kama mtoto kaumiza kichwa na kaja na wazo zuri ambalo linahitaji usaidizi toka kwako mzazi basi ni vyema ukamsaidia.
Kama mzazi hupendi kuona mwanao anataambika...ni ule upendo wa asili wa mzazi. Hivyo basi tumia mali zako katika kumsaidia mwanao kupata mali zake.
Kama mtoto umemlea vizuri sidhani kwamba kumwambia mwanangu hizi mali zote nizochuma ni za kwetu sote hivyo nataka wewe uzitumie kuendeleza utajiri wa familia kutamfanya abweteke but rather itamfanya atambue kuwa ana jukumu kubwa na kwamba mzazi wake anamtegemea na kuthamini uwepo wake katika familia.
Atapata ama akipata mchumba atajilipua kuwa huyu huyu ndo wife material jamani. Rangi inavutia ile emotions zikiwa zinafanya kazi na zime overtake cortex brain hutaelewa mpaka ziishe.Binti mwenyewe pisi fulani anaonekana
Kwa tukio alilofanya unaweza kushangaa
Mali hizi zitawatoa roho watu
Ova
Wachagga Mali zilishawatawala ! Endeleeni kuuana tu.
MOSHI: BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI ILI ARITHI MALI, MWILI WAGUNDULIWA BAADA YA MWAKA MMOJA
• Meya Juma Raibu ashindwa kujizua amwaga machozi na kulaani vikali, awaasa vijana kuacha tamaa na starehe
•Meya Raibu ampongeza Rpc Kilimanjaro ACP Simon Maigwa na timu Yake Kuendelea Kusikiliza Na Kutatua Jinai Mbali Mbali
Ikiwa zimepita siku kadhaa toka litokee tukio la kijana mmoja jijini Arusha kumuua mama yake mzazi Kwa tamaa ya Mali, Limegundulika tukio lingine la kinyama mkoani Kilimanjaro katika Manispaa ya Moshi ambapo binti mmoja aliejulikana Kwa jina Moja la Wendy amemuua Mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambae ni Nesi mstaafu wa Hospital ya KCMC.
Jeshi la Polisi limeufukua Mwili huo leo tarehe 09-01-2022 katika kata ya Rau baada ya kumhoji binti huyo Kwa zaidi ya wiki mbili sasa Kisha kukiri kumchinja mama yake Kwa panga na kumfukia nyumbani hapo.
Ni takribani Mwaka sasa ndugu na majirani walipokuwa wamuulizia mama huyo walipatiwa majibu na binti huyo kuwa amesafiri Kwa matibabu nje ya nchi.
Akizingumza Kwa uchungu huku akilengwalengwa na machozi Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ndg Juma Raibu ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho na amelaani vikali tabia ya vijana kuendekeza tamaa na kukosa uvumilivu wa utafutaji Mali Kisha wanaishia kufanya matendo ya kinyama.
Namnukuu
"Kiukweli hili ni tukio la kutisha, nitoe pole Kwa familia ndugu na majirani wote mliofika hapa, nimepata huzuni sana kuona jinsi gani ya taamaa Mali imetufikisha hapa, nalaani na ninatoa wito Kwa vijana wenzangu wote nchini kuacha kupaparikia Mali na starehe mwisho wake tunageuka kuwa wanyama kiasi hiki, yaani unamuua mama mzazi?
Hivi unakuwa huoogopi laana na adhabu ya mola? nalipongeza Jeshi letu la Polisi Kwa hatua hii nawatia Moyo mwendelee na kazi hii njema ya kufichua na kudhibiti wahalifu wa namna hii na wanaoshirikiana nao".
mwisho wa kunukuu.
Tayari madaktari wameanza kufanyia uchunguzi wa postmortem Mwili huo kwajili ya hatua zinazofuata.
#MoshiBlog UpdatesView attachment 2075108
View attachment 2075109