Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Hivi unafikiriaje kumuua mtu kisa mali halafu unatoa majibu mepesi eti amesafiri au hajaniaga unahisi binadamu watakuelewa, huu uongo una mwisho.

Ni bora ukishafanya ujinga wako uende ukatoe taarifa police kua haonekani na umejaribu kumtafuta kwa kila njia humpati.
 
Mama alikuwa nesi???kcmc!

Matukio mengine tusiangalie upande mmoja...
Inawezekana kua ni kweli lakini kwa jicho la kibinadamu lawama lazima ziende kwa binti lakini je huyo mama alikua na mtoto mmoja tuu kiasi cha kufanya tukio na asijulikane?

Uhusiano wake na majirani upo je?
 
Kama ulishawahi kuishi Moshi na Wilaya zake....ukitazama kwa umakini harakati za Wana jamii, haiba na mienendo ya Wana jamii waliokuzunguka na mitazamo yao juu ya maisha unagundua kuwa kuna tatizo mahali...
Umesema ukweli na uhalisia.

Zimebaki sifa tu.

Sasa hivi mtu akifa huwezi kukuta hata wanahuzunika na kulia. Ni kunywa pombe na nyama.

Ni fursa kwa kwenda mbele, watu wanaangalia kaacha nini na kwa nani.

Migogoro ya vihamba na mali ni kama maji ya kunywa.
 
Mama alikuwa nesi???kcmc!

Matukio mengine tusiangalie upande mmoja...
Inawezekana kua ni kweli lakini kwa jicho la kibinadamu lawama lazima ziende kwa binti. Lakini je huyo mama alikua na mtoto mmoja tuu kiasi cha kufanya tukio na asijulikane?

Uhusiano wake na majirani upo je?
 
Wee sema hivyo tuu....sasa mali umahangaika kuzipa ila kwa sababu ya uchoyo watoto wako wenyewe wanakuondoa. Wazazi acheni ubinafsi gaweni mali hizo
Ila weeh jamaaa😆😆😆😆 imekuwa fundisho maana Mie ni Yule mzazi ninayewaambia watoto hizi zangu, watafute zao
 
Ila weeh jamaaa😆😆😆😆 imekuwa fundisho maana Mie ni Yule mzazi ninayewaambia watoto hizi zangu, watafute zao
Ndio ukae kimachale mzeya usije jikuta wamekukata mapanga.
Wakalishe chini waambie jamani eeh mie baba yenu nimepambana mpaka kifika hapa sasa na nyie tumieni hizi mali nilizonazo kuleta nyingine ili kama familia tuendelee kuneemeka.
 
Ila weeh jamaaa😆😆😆😆 imekuwa fundisho maana Mie ni Yule mzazi ninayewaambia watoto hizi zangu, watafute zao
Nikiona mtu anahangaika na urithi huwa namdharau! Nashukuru Babu yangu alituasa kuwa tusirithi na katika ukoo wetu mtoto huwa ni caretaker wa mali za wazazi! Tunaambiwa tutafute mali zetu. Babu hakurithi, mimi sikurithi na watoto wangu wana pesa zao kunizidi
 
Nikiona mtu anahangaika na urithi huwa namdharau! Nashukuru Babu yangu alituasa kuwa tusirithi na katika ukoo wetu mtoto huwa ni caretaker wa mali za wazazi! Tunaambiwa tutafute mali zetu. Babu hakurithi, mimi sikurithi na watoto wangu wana pesa zao kunizidi
Na hii ndo inatakiwa kufanyika kwa familia zote!!
 
Kwani mulitafuta hizo mali pamoja na mzazi? Mzazi yuko sahihi kabisa, yeye ndiye aliyefanya kazi na kuteseka kwa hivyo hicho alichofanikiwa kukichuma ni chake.
Kwani kuna mtu anabisha kwamba mali umeifanyia kazi? Yaani wee kwa sababu uliteseka basi wataka na mwanao pia ateseke kupata mali kama ulivyoteseka wewe....huo ujinga bwana. Mali zako mzazi zinapaswa kumrahisishia mwao kupata zake.

Kama mtoto umemlea vizuri atathamini mali za mzazi wake na akiona kuwa mzazi ana moyo mkunjufu katika kumshirikisha mwanae katika usakaji wa hizo mali na kwamba zina mchango wa moja kwa moja katika kumuendeleza yeye sidhani kama itafikia hatua ya yeye kuanza kuwaza kukukata mapanga
 
Yaan mzazi kakukuza plus kukusomesha pengine kajinyima ili mwanae akuhudumie mpaka sasa umekuwa jitu lizima yaani fadhila zote hizo bado unasema ni mbinafsi aisee utakuwa una matatizo ya akili.
Hayo yote kwanza ni wajibunwa mzazi usianze kusemankuwa ni fadhila. Wee unaleta mtoto duniani hujui kuwa ni jukumu lako kumlea mpaka awe mkubwa na anajitegemea?

Tena as a matter of fact mpaka mtoto anafikia hatua ya kukuua mzazi means wewe kama mzazi ulishindwa kumlea vizuri huyo mwanao.

Nakwambia hivi nikiwa na background ya criminal psychology, mtoto mpaka kifikia kumua mzazi kuna sehemu mzazi alishindwa majukumu yake kama mzazi.

Dunia ina wazazi wakipuuzi sana ambao hawakustahili kuwa wazazi to begin with.
 
Back
Top Bottom