Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Zaidi ya wanafunzi 50 wa Shule ya Sekondari ya Kaloleni Islamic ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kuungua na moto baada ya bwenì walilokuwa wakiishi kulipuka moto leo saa saba mchana.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto katika bweni hilo la wasichana lenye vyumba 20.
Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni wanafunzi wa chumba cha tatu ndani ya bweni kilicholipuka moto kuwa na vifaa vinavyolipuka.
Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jeremiah Mkomagi amesema hakuna majeruhi yaliyojitokeza licha ya vifaa vya wanafunzi yakiwamo madaftari, magodoro.
Kaloleni Islamic Seminary imekuwa na historia ya kuungua ikiwa ni mara ya pili kupatwa na janga la moto.