GE2025 Moshi mjini Tunahitaji Kiongozi wa Kweli, Sio Mtumwa wa Makundi!

GE2025 Moshi mjini Tunahitaji Kiongozi wa Kweli, Sio Mtumwa wa Makundi!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Joined
Jul 27, 2024
Posts
35
Reaction score
13
Moshi mjiniTunahitaji Kiongozi wa Kweli, Sio Mtumwa wa Makundi!

Katika kipindi hiki muhimu cha siasa, Moshi inahitaji Mbunge mwenye uzoefu, uwezo wa kiuongozi, rekodi ya utendaji uliothibitishwa, na moyo wa dhati wa kuwatumikia wananchi, si mtu anayesukumwa na makundi ya kimaslahi au ajenda binafsi.

Mhe.PRISCUS TARIMO @⁨Priscus Tarimo B⁩ Mbunge wetu wa sasa amethibitisha kwa vitendo kuwa ana sifa hizo zote Ameonesha uongozi wa haki, uwazi, na matokeo si kwa maneno bali kwa kazi halisi zilizogusa maisha ya wanaVunjo na zinazoonekana....

Tunaendelea kumuombea kwa Mungu azidi kumpa afya, busara, na nguvu ili atuvushe tena kwa mafanikio makubwa zaidi..

Moshi Inasema: "Tumeona Matokeo, Tunataka Muendelezo!"

PRISCUS TARIMO AMEFANYA NA ZIADA INGINE ATAFANYA KIPINDI CHA 2025-2030

By Mwan
IMG-20250718-WA0004.jpg
dishi Bora
 
MBUNGE APOTOSHA UMMA

TUMSIKILIZE MBUNGE MSOMI PRISCUS TARIMO BINGWAA

KATIKA MIFANO YA KAZI ALIZOFANYA MBUNGE ZIMEPOTOSHWA KAMA ILIVYOJIELEZA HAPO CHINI.

"MBUNGE HUYU HAINA HAJA YA KUDANGANYWA KUHUSU UTENDAJI WAKE BALI TUTIZAME SEHEMU KADHAA KISHA TUJIULIZE KABLA HAJAWA MBUNGE ZILIKUWAJE NA SASA ZIKOJE MFANO:- "

1. HOSPITAL YA MAWENZI- Hii ni Hospitali ya Mkoa ambayo Utaratibu wa ujenzi na ukarabati huratibiwa na ofisi ya mkoa, Tamisemi na wizara ya afya na sio ofisi ya Mbunge hivyo hizi ni kazi za Rais na sio Mbunge. Hapa tumedanganywa, ST.JOSEPH hii ni hospital ya Binafsi ya Dini ambayo mbali na kujifanyia maendeleo yake binafsi bado anadaiwa mil. 13 ambayo hayailipa hadi Sasa. NA KCMC hii ni Hospital ya KKKT na Serikali ni kama mbia. Hospital hii ni hospital y Rufaa ambayo utaratibu wa ujenzi na ukarabati uko chini ya wizara na sio ofisi ya jimbo. Mbali na kanisa kujiendeleza serikali kuu kupitia Rais amesaidia uboreshaji na ujenzi wa majengo kadhaa na sio mbunge. Hapa pia Mbunge katudanganya.
2. SOKO LA MBUYUNI - Soko la mbuyuni limejengwa na fedha za ndani na hii ni baada ya soko kuungua na serikali kuwaahidi wafanyabiashara kuwajengea soko. Ikiwa Mbunge kahusika na ujenzi wa soko hili, inatakiwa atueleze je ujenzi huo umetumia bil. 2, na ikiwa yeye mbunge kahusika mbona vibanda 14 ambayo viko tayari wamewanyima wahanga kwa kuwapandishia kodi kuwa 300,000/= na vingine kuwagawia watu wasio wahanga kama Gadafi wa CCM na mbona vibanda mzunguko hadi sasa inasemekana viongozi hao wawakilishi wamevigawana hata kabla ya kuanza ujenzi. Mbunge atueleze ikiwa ni yeye kasimamia ujenzi huu basi anahusikaje kwenye haya madudu.
3. MASHULE YA SECONDARY ya Lucy Lameck ilianza kupigiwa kelele na Diwani Mosha 2016 hadi Aliyekuwa katibu wa CCM kipindi hicho Kataba kumuunganisha na Watu wa Tamisemi hili ni jasho la Mosha Diwani Majengo
4. BARABARA- barabara nyingi zilizojengwa kipindi chake ni za chini ya kiwango mfano Barabara ya ANNA Mkapa Sekondary, barabara ya Kili Fm - Soweto
5. UJENZI WA OFISI ZA KATA - Ujenzi wa ofisi za Kata ni nchi nzima na hazina mahusiano na uwepo wa Mbunge kwani haikuwa moja ya ahadi bali mipango ya Halmashauri
6. UJENZI KITUO CHA AFYA PASUA- kituo cha afya Pasua kilijengwa 2016 na kuzinduliwa 2018 na Rais wa Sasa akiwa Makamu wa Rais na kumsifia Juma Raibu katika hafla hiyo iliyofanyika ofisi ya CCM kata ya Bomambuzi.
7. UTOAJI WA PIKIPIKI JESHI LA POLISI - PIKIPIKI ZILE NI ZA ABIRIA HAZINA WEZO WA KUFUKUZANA NA WAHARIFU
8. NENDA ZIMAMOTO GARI ZIKO PALE - Gari za Zimamoto zilitolewa kwa Mkoa wa Kilimanjaro na hii ilikuwa ni ombi la mkuu wetu wa Mkoa
9. GARI ZA KUBEBA WAGONJWA NA GARI YA KUBEBA STAFF MAWENZI HOSPITAL - Gari hizi zimetolewa na Serikali kuu kwa hospital zote za Mkoa ikiwemo Mawenzi na sio kazi ya Mbunge. Rais apongezwe kwa kazi nzuri
10. N.K- TUNAOMBA MAJIBU YA MAMBO YAFUATAYO.
1. UJENZI WA HOSPITAL YA WILAYA UMEKWAMA WAPI
2. UJENZI WA UWANJA WA NDEGE MBONA UMESIMAMA
3. UJENZI WA STEND YA MFUMUNI UMEKWAMIA WAPI
4. BARABARA YA KILIFM SOWETO MBONA IMESIMAMA
5. AHADI YA UJENZI WA SOKO LA MANYEMA UMEKWAMIA WAPI
6. MADENI YA VIKUNDI NA TAASISI YATALIPWA LINI MAANA UBUNGE UNAKOMA BAADA YA SIKU 3 ZIJAZO.

By ✍🏾Mwandishi Bora
 
Back
Top Bottom