Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Libya

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2016
Posts
790
Reaction score
1,968
Wagombea wa CHADEMA Moshi wakataliwa kupokelewa fomu zao na Mkurugenzi.
======

Mkurugenzi amegoma kupokea fomu baada ya tuhuma za awali kwamba sio halisi na kutaka kabla wahusika hawajazirudisha wakathibitishe polisi kama ni halisi ama La.

Baada ya katibu wa CHADEMA kuhoji iwapo vyama vyote vinaenda polisi kuthibitisha, amejibu yeye aliemtuhumu na wote waliomtuhumu ndio wanatakiwa kwenda polisi kuzithibitisha kabla hawajazileta kwake.

Pia katibu wa CHADEMA alilalamikia kuwa na risiti za aina mbili kwa wagombea wa CCM na CHADEMA ambapo risiti za CHADEMA zimekuwa printed kwenye computer ilhali za CCM ni stakabadhi ya halmashauri.

Kuhusu hilo mkurugenzi, amemtaka kuwasilisha kwa maandishi malalamiko yao na yeye atakaa na wataalam kuangalia kipi ni kipi lakini amesema uko utata, zipo ambazo ni stakabadhi kama za mahakama, nyingine za mfumo na nzuri ni ya stakabadhi lakini wakitaka majibu wawasilishe malalamiko yao.

Pia mwenyekiti amelalamika suala la risiti ya mgombea ubunge kuandikwa ni ya mgombea udiwani, mkurugenzi ametaka wayawasilishe wamalizane.


=====

Kwa upande wake mkurugenzi amesema ametoa fomu halali na CHADEMA wakaandika barua na kumpelekea wakimtuhumu amewapa fomu zisizo halisi na baadae kwenda polisi. Ikabidi awaandikie kwamba hilo suala halina shida lakini kwa kuwa wameenda polisi, yeye hana uweza wa kutambua kitu 'fake' hivyo watafute mamlaka yenye weledi wa kutambua hivyo asingeweza kuzipokea.


 
Sasa mkurugenzi kakosea nini hapo?

Wewe unapewa fomu kisha unasem ni feki halafu unataka uirudishe kwa aliyekupa fomu feki tena.

Huyo jamaa wanayemuita katibu analisauti likubwa tu na anaongea saana ila kichwani hamna kitu.

Hata mimi nisingeipokea...nenda kqnishtaki nimekupa fomu feki...ili nishtakiwe kwa kujaribu kukurubuni.
 


CHADEMA wataka TUME YA UCHAGUZI kumuondoa msimamizi wa uchaguzi Moshi Vijijini ambaye ni mkurugenzi wa wilaya Castory Msigala kwa vile hawana imani naye kutokana na matendo na mienendo yake ktk kazi ya kusimamia mchakato mzima wa kuelekea katika kufanyika uchaguzi mkuu ulio wa haki na huru oktoba 2020.

Mfano fomu walizopewa CHADEMA zinautofauti mkubwa na zile fomu walizopewa wagombea wa CCM.

Risiti kwa ajili ya malipo walizopewa CHADEMA kwa ajili ya fomu zinautofauti na risiti walizopewa CCM kwa ajili ya kufanyia malipo.

Mkurugenzi amekiri fomu zina utofauti na mkurugenzi hana uwezo wa kutambua fomu halali au la.

Chanzo: Mwananchi digital
 
Back
Top Bottom