Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mzee mwenye umri wa miaka 71, Patrick Malya amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha mirungi, akiwa ni mshtakiwa wa kwanza mwenye umri mkubwa kuhukumiwa kwa kosa la mirungi.
Adhabu hiyo imetolewa wakati Mkoa wa Kilimanjaro, hasa Wilaya za Rombo, Moshi, Hai na Mwanga zikitikiswa kwa biashara ya mirungi inayoingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya, kupitia njia za panya zilizopo mpakani katika wilaya hizo.
Katika hukumu ya kesi hiyo, Jaji Emmaculate Banzi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyoketi Moshi, alimwachia huru mke wa mzee huyo, Paulina Mallya (60) kwa kukosekana ushahidi dhidi yake.
Awali upande wa mashtaka ukiongozwa na mawakili Agatha Pima na Nitike Emmanuel kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), waliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 20, 2017 katika Kijiji cha Kiboro wilayani Rombo.
Akisoma hukumu hiyo juzi, Jaji Banzi alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka, ulikuwa mzito na haukuacha mashaka dhidi ya mzee Mallya na kuukataa utetezi wake kuwa alijua amebeba mchicha na siyo mirungi.
Kulingana na ushahidi huo, Machi 19, 2017, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo alipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mzee huyo kwa kutumia gari lake aina ya Toyota Corolla T 344 CAQ amekuwa akisafirisha mirungi.
Mkuu huyo wa wilaya akamwagiza Katibu Tawala wa wilaya (DAS), Abubakar Assenga, akutane na mkuu wa kituo (OCS) cha Wilaya ya Rombo na kupanga namna watakavyoweka mtego utakaofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa.
Siku iliyofuata maofisa hao wakiwa na polisi wengine wawili, walifika eneo hilo la Kiboro saa 10:30 alfajiri na gari hiyo ilifika na kusimamishwa ambapo mshtakiwa aliamriwa afungue buti ya gari yake ili ikaguliwe ambapo alidai ni mbovu.
Gari hiyo ilipelekwa kituo cha Polisi Rombo ambapo alitafutwa askari wa kikosi cha usalama barabarani ambaye aliifungua buti bila tatizo na kukuta mifuko minne ya sandarusi ikiwa na mirungi yenye uzito wa kilo 83.
Katika utetezi mkewe alikiri mumewe kupakia mizigo njiani ingawa hakufahamu ilikuwa ni mizigo gani, utetezi ambao uliishawishi Mahakama kuwa hakuwa anafahamu jambo hilo hivyo kumwachia huru.
Kwa upande wake, Mallya alijitetea kuwa mzigo huo alipewa na mtu njiani wakati anatoka Rombo kwenda Arusha na alihisi ni mchicha au miche ya miti na alilipwa Sh200,000 za usafiri.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Banzi aliukataa utetezi huo akisema alifahamu alichokuwa amebeba kwa kuwa anakiri kulipwa Sh200, 000 akisema kama ingekuwa ni mchicha fedha hizo ni nyingi kwa mwaka 2017.
Mbali na hoja hiyo, lakini Jaji alisema mshtakiwa alikuwa ametiliwa mashaka muda mrefu kuwa anajihusisha na usafirishaji wa mirungi na hata alipokamatwa na kutakiwa kufungua buti, alitoa visingizio kwa kuwa alijua alichokuwa amebeba.
Jaji Banzi aliagiza pia kutaifishwa na Serikali kwa gari lililotumika kusafirisha dawa hizo.
Hukumu hiyo ni ya kwanza kutolewa kwa mtu mwenye umri mkubwa mkoani Kilimanjaro, ambapo kama hatokata rufaa na kuachiwa huru atatoka gerezani akiwa na umri wa miaka 85 kama atakuwa na tabia njema na kupunguziwa moja ya tatu ya adhabu hiyo.