Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Hii ni habari ya UWONGO WA MCHANA.Mwezi ulipita yaani September,ilitimia miaka 34 tangu kiongozi wa kanisa katoliki kwa wakati huo Papa John Paul II afanye ziara yake nchini.
Hakuna ubishi ya kuwa Papa John Paul II ndio Papa maarufu na aliyependwa zaidi kwa miaka ya hivi karibuni.
Sasa basi mwaka huo wa 1990,mwezi september Papa alizuru Tanzania,iliyokuwa chini ya utawala wa Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Miezi sita kabla ya ziara kanisa pamoja na serikali walifanya maandalizi kabambe,nyimbo zilitungwa na makanisa pamoja na wasanii na kupigwa radio Tanzania,zingine ziligeuka kama Anthem,bado nazikumbuka mpaka leo.
Kipindi hicho dampo la jiji la Dar Es Salaam lilikuwa Tabata,karibu na Kigogo..
Kuna watu wanadhani barabara ya Mandela ndio imetenganisha Tabata na Kigogo la ashaa,Tabata na Kigogo vimetenganishwa na mto ambao siukumbuki jina lake ila unamwaga maji yake mto Msimbazi.
Sasa basi mida ya Alasiri ndege aina ya Boeing Air Bus ilitua katika ardhi ya Tanzania,Papa alipokewana Mwalimu Nyerere waliingia katika gari la wazi aina ya Rollys Royse walipungia maelfu kwa maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na wageni waliotoka mikoani kuja kumlaki kiongozi huyo.
Msafara ulipita Pugu Road,(nyerere road),ulipofika Tazara ukakunja kushoto kuelekea Mandela Road,kumbuka wapo kwenye gari ya wazi,sasa ile kufika Tabata Matumbi,moshi mzito toka dampo ulifunika barabara yote mpaka eneo la Garage ya Auto Mech,meter karibu 400 ni moshi mzito kwelikweli.
Wale wazee Nyerere na Papa John Paul bila shaka walipata sintofahamu ya kiafya.
Haikuchukua muda dampo likahamishiwa Vingunguti na baadae Pugu
Kwanza ni kwamba babara rasmi ya wageni wa Ikulu hadi maka 1990 ilikuwa ni Puhu Road (siku hizi Nyerre Rd), then Port Acess (siku hizi Mandela Rd) halafu Uhuru Road. Ikifika Cloctower inapita Railway Street halafu City Drive (siku hizi Sokoine Rd) then Ikulu. Kwahiyo issue ya kupita Tabata ni fabrication tu
Niinaikanusha kwa nguvu zote. Mimi nilikuwa na umri wa miaka 30 wakati huo na kazi yangu ilikuwa ni maeneo ya Pugu Road. Nilifunga Ofisi kuznzia saa 8 na kwenda Buguruni Polisi. Msafara wa Papa John Paul II ulipita mida ya saa 10-11 za jioni na ulipotoka Pugu Road ni kweli ulikata kushoto kuja Buguruni. Kisha ulipofika Buguruni Mataa ukakata kulia kuingia Barabara ya Uhuru. Nami nilimshudia papa John Paul II nikiwa pembeni ya Polisi Buguruni akiwa kwenye gari ya wazi pamoja na Cardinal Rugambwa. Ila kwenye msafara naye Rais Mwinyi na Nyerere walikuwapo.
Habari za Tabata ni za UWONGO.