BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Walioachiwa huru ni Erick Teete, Fadhili Mohamed, John Daniel, Nassoro Nassoro, Paschal Mushi, Ibrahim Mkindi, Robert Massawe na Juma Hamis Ramadhan.
Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Moshi dhidi ya watuhumiwa walioshtakiwa kwa mauaji ya walinzi wa kampuni ya Utalii ya Ahsante Tours pamoja na uporaji wa Tsh. Milioni 65.5 Julai 3, 2016.
Watuhumiwa wameachiwa huru baada ya Jaji Adrian Kilimi kuukataa ushahidi wa Jamhuri wa maelezo ya Onyo na Video zilizorekodiwa na Polisi akisema Ushahidi wa Jamhuri ulitakiwa kuungwa mkono na Ushahidi Huru na hivyo Jamhuri imeacha mashaka kwa kushindwa kuthibitisha Mashtaka.
=========================
Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, imewaachia huru washitakiwa wote wanane waliokuwa wakituhumiwa kwa mauaji ya walinzi wa kampuni ya kuhudumia watalii ya Ahsante Tours, mauaji ambayo yaliambatana na uporaji wa Sh65.5 milioni.
Mauaji na uporaji huo wa fedha zikiwamo Dola 23,300 za Marekani na Sh15 milioni za Tanzania, yaliyotokea Julai 3, 2016 yaliutikisa mji wa Moshi kutokana na kampuni hiyo kuwa ya pili kwa ukubwa, ikitanguliwa na kampuni ya Zara Tours.
Walioachiwa huru na Jaji Adrian Kilimi, ni Erick Teete, Fadhili Mohamed, John Daniel, Nassoro Nassoro, Paschal Mushi, Ibrahim MkindI maarufu kwa jina la Ibra, Robert Massawe maarufu kwa jina la Kipara na Juma Hamis Ramadhan.
Upande wa mashitaka ulikuwa unadai kuwa siku ya tukio huko eneo la Shanty Town katika Manispaa ya Moshi, washitakiwa waliwaua kwa makusudi na bila uhalali, Dominic Cheddy na Omary Idd Amin waliokuwa walinzi wa Ahsante Tours.
Maelezo ya tukio hilo yaliyowasilishwa mahakamani ni kwamba siku ya tukio marehemu hao walikuwa wakitekeleza jukumu lao la ulinzi, ndipo usiku wa siku hiyo washitakiwa walidaiwa kuvamia ofisi hiyo na kupora fedha hizo.
Ni katika kipindi hicho cha uporaji, ndipo washitakiwa walidaiwa kuchukua maamuzi ya kuwaua walinzi hao baada ya kubaini kuwa mlinzi mmoja alikuwa amemtambua mmoja wao hivyo kuhofia kuwa angewataja washitakiwa.
Miili ya walinzi hao iligunduliwa asubuhi ya saa moja na katika upelelezi wa Polisi, ndipo mshitakiwa wa pili, Fadhil Mushi alikamatwa na katika mahojiano ilielezwa kuwa alikiri kushiriki mauaji hayo na kuwataja washitakiwa wenzake hao saba.
Ilielezwa na mashahidi wa upande wa mashitaka kuwa katika mahojiano polisi wakati wa kuchukua maelezo yao ya onyo, washitakiwa wote walikiri kufanya mauaji hayo na washitakiwa wanne, mbali na maelezo walichukuliwa video.
Washitakiwa hao ni mshitakiwa wa kwanza, Erick Teete, wa pili, Fadhili Mohamed au Mushi, wa tatu, John Daniel na mshitakiwa wa 7, Robert Massawe au Kipara na katika kuthibitisha shitaka, Jamhuri iliita mashahidi 13 na kuwasilisha vielelezo 15.
Vielelezo vilivyowasilishwa kortini ni pamoja na maelezo ya onyo ya washitakiwa wote wanane, ripoti za uchunguzi wa miili ya marehemu (postmortem report) na baada ya kusomewa mashitaka yao, washitakiwa wote wanane waliyakanusha.
Ushahidi wa Jamhuri ulivyokuwa
Mmoja wa mashahidi ni aliyekuwa mkuu wa Upelelezi (OC-CID) wilaya ya Moshi, Elias Haway ambaye alieleza namna alivyopata taarifa za uwepo wa tukio hilo na baadaye Agosti 28, 2016 alipata taarifa mtuhumiwa mmoja yuko Arusha.
Alituma timu ya makachero ambao walifanikiwa kukamata baadhi ya washitakiwa ambao ni mshitakiwa wa 7 (Kipara), na mshitakiwa wa kwanza (Teete) ambao katika mahojiano na polisi walikiri kushiriki tukio hilo na kutaja washirika.
Katika ushahidi wake huo, shahidi huyo alieleza kuwa mshitakiwa Robert Massawe alimtaja Erick Tetee, Nassoro Nassoro, Juma Hamis na Ibra wakati Tetee waliwataja Massawe au Kipara, Nassoro Nassoro, Big na Ibrahim Mkindi.
Mashahidi wengine wanane ambao ni maofisa wa polisi, ushahidi wao ulikuwa hautofautiani na wa bosi wao na kwa sehemu kubwa walieleza walivyokagua eneo la tukio, kukamata washitakiwa na kuandika maelezo yao ya onyo.
Raia pekee waliotoa ushahidi wao ni Dk Patrick Amsi aliyefanya uchunguzi wa miili ya marehemu, Tom Swai aliyekuwa mtunza stoo Ahsante Tours na Gilbert Shangali aliyekuwa meneja walioeleza walivyokuta ofisi zao zimevunjwa.
Utetezi wa washitakiwa
Mshitakiwa wa kwanza, Eric Teete alikanusha mashitaka hayo akisema alikamatwa Agosti 25, 2016, alikamatwa kutokana na ugomvi uliotokea siku hiyo eneo la Ilboru kati yake na askari aitwaye Hamis aliyeahidi kumlipizia kisasi.
Alishangaa siku hiyo saa 5:00 usiku mlango ukigongwa na waliingia maofisa watano wa polisi ambao walimchukua hadi kituo cha Polisi Arusha ambapo siku iliyofuata alihamishiwa kituo kikuu cha Polisi Moshi na kushitakiwa kwa mauaji.
Mshitakiwa wa pili, Fadhil Mohamed, alidai alikamatwa na Polisi Jijini Arusha Agosti 26,2016 wakati akiuza viatu ambapo polisi walimshuku labda vimeibwa mahali, ndipo akakamatwa na kufungwa kitambaa cheusi usoni.
Anadai kilipofunguliwa, alijikuta yuko kituo kikuu cha Polisi Moshi ambapo alipelekwa katika chumba cha mateso na kuteswa na kulazimishwa kusaini karatasi alizoletewa na polisi na kama asingefanya hivyo wangemuua.
Mshitakiwa wa tatu, John Daniel alisema yeye alikamatwa Septemba 2, 2016 wakati anasafiri kutoka Arusha kwenda Moshi na polisi walipompekua walimkuta na msokoto mmoja wa bangi, alipelekwa chumba cha mateso na kuteswa.
Huko kama mshitakiwa mwenzake alitakiwa kusaini karatasi zilizoandikwa na alizisaini baada ya kudai kuteswa, huku mshitakiwa wa 4, Nassoro akidai alikwenda kituo cha Polisi Moshi kumdai koplo Charles nguo zake, akashangaa amekamatwa.
Kwa upande wake, mshitakiwa wa tano, Paschal Mushi alijitetea kuwa alikamatwa Agosti 22, 2016 huko Majengo akituhumiwa kuwa na mali ya wizi na alipopelekwa kituo kikuu mjini Moshi, alidai aliteswa na kutakiwa kusaini karatasi ambazo hakuzielewa.
Mshitakiwa wa sita, Ibrahim Mkindi yeye alidai kukamatwa Agosti 28, 2016 eneo la Kaloleni Moshi na kupelekwa katika chumba cha mateso ambapo kama wenzake, alitakiwa kusaini karatasi zenye maelezo na kudai kuwa alizisaini kutokana na kipigo.
Kwa upande wake, mshitakiwa wa saba, Robert Massawe alijitetea akidai kuwa alikamatwa Agosti 24, 2016 huko Arusha na kusafirishwa hadi Moshi na kupelekwa chumba cha mateso akitakiwa kusaini karatasi fulani na kudai alilazimika kuzisaini.
Mshitakiwa wa 8, Juma Ramadhan alidai Septemba 4, 2016 usiku wa manane alikamatwa na polisi nyumbani kwake akiwa na bangi ambapo alipelekwa chumba cha mateso na kudai kuteswa ili asaini karatasi fulani, na ilimlazimu kuzisaini.
Hukumu ya Jaji Kilimi
Katika hukumu yake hiyo jaji aliukataa ushahidi huo wa maelezo ya onyo ya washitakiwa na mikanda ya video iliyorekodiwa na maofisa wa Polisi akisema ushahidi wa namna hiyo ulitakiwa uungwe mkono na ushahidi huru.
“Nakubaliana na upande wa utetezi katika majumuisho yao ya mwisho kuwa hakuna shahidi hata mmoja aliyetoa ushahidi kwamba alishuhudia mauaji haya hivyo ushahidi wote wa kesi hii ni wa kimazingira,” alisema Jaji Kilimi.
Jaji Kilimi alisema maelezo ya onyo ya ungamo ya mshitakiwa mmoja kama yanamhusisha mshitakiwa mwingine hayawezi kuchukuliwa kuwa ni ushahidi umeungwa mkono lazima upatikane ushahidi mwingine unaounga mkono.
Ni kutokana na kutopatikana ushahidi huru wa kuunga mkono maelezo ya onyo ya washitakiwa na video walizorekodiwa, Jaji alisema upande wa ushahidi wa upande wa mashitaka, umeshindwa kuthibitisha shitaka hilo na kuacha mashaka.
MWANANCHI