Moshi: Waliotuhumiwa kuua walinzi wa Asante Tours na kupora Tsh. Milioni 65 washinda kesi

Nani atakuwa mlinzi wa walinzi wetu!
 
Polisi wana weledi mdogo sana au hawapendi kuhangaika kupata ushahidi ndio maana wanafanya makosa ambayo wanashindwa kuwatia watu hatiani.

Wao wakikamata mtu wanataka wamtese ili asaini hayo makaratasi yao basi wawe wamemaliza kazi,sasa mtuhumiwa anaweza kukubali tu kusaini ili asiteswe Ila akifika mahakamani anakataa anasema nililazimishwa.

Kama hawa watuhumiwa ndio waliohusika kuua,kwanini ushahidi umekosekana?Je hawakukutwa na pesa zilizoibwa?bunduki ilitumika?taarifa gani iliwafanya polisi wawakamate hawa watu na si wengine?
 
Upande Jamhuri hususan wa mawakili wasomi wa serikali ofisi ya DPP / NPS wapikwe vizuri kitaaluma ili kulisaidia jeshi la Polisi ili haki iweze kupatikana inapostahiki.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA​


Mkurugenzi wa Mashtaka​

MKURUGENZI WA MASHTAKA
Mkurugenzi wa Mashtaka ni mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mkurugenzi wa Mashtaka ndiye msimamizi mkuu wa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Mawakili wa serikali na Waendesha Mashtaka katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:
  • (i)Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
  • (ii)Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
  • (iii)Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
  • (iv)Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
  • (v)Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
  • (vi)Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenyetija katika mashtaka ya jinai;
  • (vii)Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
  • (viii)Kuteua na kutenguamamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
  • (ix)Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masualaya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
  • (x)Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
  • (xi)Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
  • (xii)Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiii)Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiv)Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
  • (xv)Kuandaa na kuwasilishakwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
  • (xvi)Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka
Source: https://www.nps.go.tz/pages/director-of-public-prosecutions
 
Kwani hapa inakuwaje? ndiyo imeisha hivo au?maana wale walinzi ilithibitika wameuawa.Au wanatakiwa warudi wakawatafute wauaji upya. Sababu kusipokuwa na action yoyote kwa uzembe kama huu. Ni rahisi sana kwa police kuchukua rushwa kutoka kwa watuhumiwa na kupindisha ushahidi.On the other hand naona mhimili wa mahakama pia ulikuwa huru kutekeleza majukumu yake.

Hapa kuna mtu anaitwa DPP,yeye anahusika wapi?
 
Aisee ..! Polisi hawa Mungu anawaona.
 
Yan hapo walikamatwa bila ushahid wa kutosha walifosi tu wasaini jau sana

JUMBA LINALODAIWA NI LA 'MATESO' A.K.A MBAO FC

(Page 23 - 24)
......taken to Moshi central Police. He further said on 28/8/2016 he was taken to torture room where he was tortured and returned to lock up, the following day he was taken in the same room, then upon being scared to be tortured again, he did sign the document given to him without knowing what is inside.

In regard to sixth accused one Ibrahim Athuman Mkindi (DW6) defended by saying that he was arrested by police officers on 28/8/2016, at Kaloleni, Moshi town. Next day on 29/8/2016, he was sent to torturing room known as Mbao FC, and forced to sign a paper which he did not know what was written on it.

He further explained the bad relation with Isack Chaula a police officer whom he owes money after contract of payment his money breached.

Then it was the seventh accused one Robert John Massawe (DW7) who said that on 24/8/2016 at 20:00 hours, he was arrested by 8 police officers having canibias satiya (Bang!) in his bag, after arrest they sent him to kwanguneme Police Post Arusha, at about 21:00 he was transferred to Arusha Central Police.

On 26/8/2016 at 18:00 hours, he was transported to Moshi by Police officers whom he mentioned to be Afande Pessa, Haway and Derick. Upon arrival at Moshi at about 21:30, he was then taken to Mbao FC .......

Source : Republic vs Erick Willson Teete & Others (Criminal Session Case 44 of 2019) [2022] 64 (14 December 2022); | Tanzlii
 
Bro walinzi walijiua wenyewe?,
Kama wao si wauaji sasa tuoneshwe wauaji,
la sivyo tutatoa hukumu huku mtaani!!
Unafahamu kazi ya Mahakama?
Bro walinzi walijiua wenyewe?,
Kama wao si wauaji sasa tuoneshwe wauaji,
la sivyo tutatoa hukumu huku mtaani!!
Hakuna shaka, kua walinzi waliuwawa. nani aliwauwa ? huo ndio msingi wakesi yenyewe.
Kama umesoma Uzi wenyewe , umeona jinsi watuhumiwa walivyo kamatwa na kuteswa Ili wakiri kosa wenyewe.

Jaji hawezi kumfunga mtu kifungo Cha maisha au amhukumu kunyongwa bira ushahidi usio acha shaka eti , kwasababu watu wameuliwa.
Ni jeshi la Polisi ndio lenye kukurupuka na kukamatwa watu ovyo na kuwabambika kesi badra ya kutumia weredi wakamate waharifu wenyewe .
 
Mshtakiwa wa kwanza namfahamu aisee! Mama yake kasota sana. Alikuwa Tour guide wa Ashanti Tours! Hongera kwa kushinda
 
Polisi warudi field kuwasaka wahalifu ili kutenda haki kwa hao walinzi
Mkuu kesi ni sayansi.

Hayo majamaa ndiyo mauwaji menyewe, isipokuwa ushahidi umeacha mwanya kwa makusudi!

Ni weledi mdogo wa wapelelezi wa Polisi ama rushwa"kuburuza" ushahidi kwa kukusanya vielelezo dhaifu na kuacha vya muhimu,.
 
Lakini Kuna wawili wamekili kukutwa na bangi, inakuwaje,?
 
Lakini Kuna wawili wamekili kukutwa na bangi, inakuwaje,?
kukutwa na bangi huwezi hukumiwa kwa madawa ya kulevya wakati kesi ni ya mauaji labda wafunguliwe kesi nyingne ya madawa ya kulevya
 
ASILIMIA kubwa ya mawakili wa jamuhuri Ni vilaza, matokeo Yake ndo haya

ASILIMIA kubwa wanaajiliwa kwa maelekezo ya vimemo,kadi ya chama[emoji26]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…