The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wazawa wanaotoka katika vijiji vya Kondeni, Mawanjeni, na Mitala wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, wameungana kwa pamoja na kuanzisha ujenzi wa barabara ya Samaria yenye urefu wa kilomita 1.5 inayounganisha vijiji hivyo.
Wakizungumza na TBC, wakazi wa vijiji hivyo wamesema awali barabara hiyo ilikuwa ikitumika na waenda kwa miguu na bodaboda, hali iliyowalazimu kutumia gharama kubwa kusafirisha mazao yao.
Kwa sasa, wakazi hao wana imani kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutawasaidia kusafirisha mazao yao kwa urahisi na kujiongezea kipato.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kirua, Edenikaria Kaale, amesema barabara hiyo imewatesa kwa muda mrefu, hasa wakati wa mvua, hivyo walijitolea kwa pamoja kuijenga.
Mhandisi mshauri wa ujenzi wa barabara hiyo, Fredrick Masawe, amesema ujenzi utagharimu shilingi milioni 87, na itajengwa kwa kiwango cha changarawe. Msimamizi wa mradi huo, John Tarimo, ameiuomba Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kutenga bajeti ya kuzitunza barabara hizi ambazo wananchi wanazijenga kwa kujitolea.
Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini wilaya ya Moshi, Mhandisi African Orota, amewataka wakazi wa vijiji kujitolea kutunza barabara ili ziweze kudumu na kuleta maendeleo.