DOKEZO Moshi: Wanufaika wa TASAF wanyimwa malipo yao kwa muda wa miezi mitano, watakiwa kukarabati barabara hadi zikamilike

DOKEZO Moshi: Wanufaika wa TASAF wanyimwa malipo yao kwa muda wa miezi mitano, watakiwa kukarabati barabara hadi zikamilike

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wanufaika wa TASAF kutoka katika baadhi ya Kata za Machame Mashariki, pia baadhi ya kata zilizopo katika Wilaya ya Moshi na Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro wamekosa malipo yao tangu kuanza kwa mwaka huu Januari hadi sasa Mei 2023.

Ndani ya hiyo kata hiyo kuna Kijiji kadhaa vikiwemo Narumu, Usari, Orori, Tela na Ulali.

Baadhi ya wanufaika hao wamesema kuwa mara ya mwisho kupata pesa yao ilikuwa mwezi wa kumi na mbili 2022, lakini hadi mwezi huu wa tano hawajapata malipo yoyote na kwamba wanaishi kwa tabu.

Wanufaika hao wamekuwa wakishurutishwa kuja na majembe kuchimba /kukarabati barabara na kwamba hadi wakamalishe kukarabati wa barabara ndipo watapata malipo yao.

Baadhi ya wazee na yatima wamekuwa wakipitia katika kipindi kigumu tangu kusitishwa kwa huduma hiyo mwishoni mwa mwaka jana hadi hivi sasa.

Helena Lelo ni mama wa watoto watatu ambae ni mnufaika wa mfuko huo anasema kuwa anapitia kipindi kigumu yeye na watoto wake kwa kuwa fedha hizo zilikuwa zinamsaidia kununua vifaa vya watoto shule pamoja na matumizi ya chakula nyumbani lakini leo hii wanaambiwa wakakarabati barabara za kijiji ndipo hela zitatoka lakini hadi sasa hakuna malipo yoyote yaliyotolewa.


Pia soma Simbachawene: Tunafuatilia madai ya wanufaika wa TASAF kutolipwa
 
Wanaoteseka ni Kaya maskini, na wazee wasiojiweza
 
Asee kule geitq hawataki huu ujinga kesho wange amka Mtendaji na jopo lake washa liwa kichwa
 
Nimeona kibao kwenye barabara moja nikashangaa tasaf imekuwaje? Ila nadhani serikali inajua.
 
Huenda hao watu walijiunga na kifurushi cha TASAF ambacho mnufaika anafanya kazi ndipo analipwa .sasa kama hakuenda kwenye kazi outomatic mfumo unakataa kumlipa na ninachofahamu kujiunga ni hiari.
 
Nilisikia hukp watu wote nu matajiri sasa TASAF ya nn tena?
 
Back
Top Bottom