Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mafuta ni hatari sana, baada ya Msamvu Morogoro sasa yamehamia Kanisani Moshi.Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha
Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.
UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.
Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.
Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer
Chanzo: Mwananchi
=====
MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO
Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi
Amesema baada ya hilo tukio wamemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer bila mafanikio. Na kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano
Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, watu wazima 16
KuzimuHuwa natamani sana siku ifike watu wajue hayo mafuta na maji yanayoitwa ya upako yanapatikana kutokana na nini
Dah ingekuaje ..huko usukumani watu wangewatania Sana eehHili tukio lingetokea usukumani hili.......sipat picha
Orodhesha hapa acha kupiga porojo za uongoAngalia hayo makanisa ya wanaojiita manabii na mitume, asilimia 95 ni wachaga.
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha
Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.
UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.
Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.
Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer
Chanzo: Mwananchi
=====
MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO
Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosid
Amesema baada ya hilo tukio wamemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer bila mafanikio. Na kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano
Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, watu wazima 16
😂😂wajinga hawawezi kuisha
Hapana mkuu hapo umedanganya. Hivi ulishawahi kusikia hata hawa wanaojiita 'manabii' hata mmoja ni mchaga?Angalia hayo makanisa ya wanaojiita manabii na mitume, asilimia 95 ni wachaga.
Wewe ni ujinga kweli kama makonda. Kwani wanaoishi Moshi ni wachaga pekee? Ukiambiwa waumini waliokufa ni makabila nje ya Kilimanjaro utashangaa?
Bwege sana wewe!
Kufa ili ukanyage mafuta ya Mwamposa ni uzembe wa kufikiri sifa ambayo sikuwahi kudhani kuwa wachaga wanaweza kuwa nayo