Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Vilio na simanzi vimetawala katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Rufaa ya mkoa Kilimanjaro, wakati ndugu wakitambua miili ya ndugu zao 20 waliofariki kwa kukanyagana usiku wa Februari 1,2020.

Watu hao walifariki kwa kukanyagana na kukosa hewa, wakati wakigombea kukanyaga mafuta yanayodaiwa kuwa na upako yaliyomwagwa na eti anaejiita mtume Boniface Mwamposa na wasaidizi wake katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Screenshot_20200202_090950.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inahuzunisha but wamejitakia wenyewe. Najaribu kufikiria jinsi makumi elfu ya watu waliofungwa na kushikwa akili zao pamoja na ufahamu wao kutokana na vitu walivyo chukua na wanavyo vitumia kutoka kwa hawa matapeli wa dini. Hiyo mafuta ni nguvu ya giza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaitwa Bulldozer huwa anafanyia kongamano TANGANYIKA PACKERS KAWE.
Na kaitwa na polisi ajisalimishe.
Poleni wafiwa.

Innalillah wainnalillah rajuun.
 
Hata mimi kwa upande wangu ninahisi kuna uzembe utakuwa umetokea, maandalizi yalikuwa mabovu au utaratibu na maelekezo kwa waumini hayakueleweka, na pia kuhusu kuondoka baada ya tukio sio sawa pia ila mimi kilicho nisikitisha watu wana-conclude kuwa Mwamposa ni nabii feki kitu ambacho ni makosa hata kwa Mungu,
Angekuwa siyo nabii feki baada ya tukio la vifo hivyo asingeondoka (tuseme asingekimbia) na kuacha miili ya waliomchangia sadaka (kondoo wake) ikiwa hata haijatolewa eneo la tukio. Umeniuliza swali hapo juu na hii ni sehemu ya majibu uliyohitaji.

Mwalimu Mwakasege mwenyewe majuzi tu akiwa kwenye mahubiri yake alifiwa na mwanae pekee mkoa mwingine lakini hakuondoka na kuwaacha solemba kondoo wake hadi pale alipomaliza kutoa huduma kwao ndipo akaenda kwenye msiba wa mwanae tena wa kumzaa.
 
Usimzungumzie shetani tafadhali

Analalamika sana huku mnamuonea
Shetani ana mbinu nyingi za kumtumia Mwanadamu ili kuthihirisha ufalme wake.
Alimtumia mzee moja wa huko Arusha akawa anatoa kikombe cha dawa ya miti maarufu kama kikombe cha Babu. Huyu naye alikuwa anatumia jina la Yesu. Sasa hivi huyu babu hatumskii tena.
Wako manabii wengi sana wa uongo hapa Tanzania ambao wanatumia Jina la Yesu Kristo.
Yesu Kikristo alisema " watakuja manabii wengi wa uongo na watatoa pepo kwa jina langu"
Ukiona muhubiri anakuwa na Kanisa lake, Mhasibu wa Sadaka ni yeye na mtunza fedha ni mke wake au binti yake ujue hiyo si kutangaza ne no la Mungu ila ni Biashara.
Kwa kifupi Ufalme wa shetani haudumu kamwe na wafuasi wake nao hawadumu kamwe,
Tujiepushe na Manabii wa Uongo.
Serikali izuie Taasisi za Dini za watu Binafsi ambazo hazina mfumo wa Kikanisa na zinakusanya sadaka na kuzitumia kwa maslahi binafsi bila kulipa kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wachaga na ujanja wenu wote tunajua mmesoma mnakamatwa vipi akili kumwagiwa chini mafuta ya alizeti eti upako.Hio miujiza ya kupata utajiri bila kufanya kazi mmetoa wapi
 
Nadhani wameharibiwa akili na CCM, nikashangaa sana walipoomba radhi kwa Mtume Yohana kwa kuwa hawakumchagua, sasa akili nazo zimepotezwa na shida nyingi
Hata uchagani wapo kumbe wajinga? Mbona huwa mnasema humu kuwa wachaga wamesoma sana? Au hawakuelimika? Pole zao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea vema sana kiongozi wangu Mungu hayuko hivyo sijui watu wanapumbazwa na nini jamani
Waganga wa kienyeji huu utawala wanakuja kwa njia ya kichungaji..zamani lete njiwa wa njano...siku hizi njoo upakwe mafuta ya majini..sijui na keki za kuzimu..ukute huu nao ni mkafara tu....hilo neno wasilitafute kwe biblia kutwa kukimbilia keki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Freemason at work ili kupooza ukali wa ishu katoa zuio la makonda akili zote ziko kwa makonda badala ya moshi
 
Kusiwe na Double Standard,Kitendo alichokifanya Mwamposa si cha kiungwana hata kidogo,waamini wake 20 wamekufa yeye amepanda ndege na kurudi Dar kwenda kawe kuhubiri,Huyo jamaa anastahili kifungo,kwanza inabidi awekwe ndani kwa usalama wake maana sie tunaamini ametoa kafara ndio maana haijamgusa kabisa,kwa usalama wake tunaomba polisi mumuuhifadhi ndani kwa mda mpaka uchungu wa kuondokewa na ndugu zetu 20 upungue.
 
Kaua ndiyo. Bila mkutano wake watu wasingekufa. Bila kuwaambia watu wakanyage mafuta,vifo hivyo visingetokea.
Hapana aisee hyo siyo sababu watu wamekanyagana kwa uzembe wao wenyewe

"Bila mkutano watu wasingekufa"
Kifo kinatokea kokote hakitabiriki n pia huo mkutano ungefanyika na asingekufa mtu na kibali cha mkutano alishapewa hiyo imetokea tu watu na umbumbu wao wakaumizana wao wenyewe kwa wenyewe

"Asingewaambia watu wakanyage mafuta"
Hapa sioni sababu kwani wangeambiwa watembee uchi upepo wa upako uwaaingie wangefanya hivyo ?...sio kila unaloambiwa unatekeleza sometimes unaweza ambiwa upuuzi ni akili kumkichwa




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom