Shetani ana mbinu nyingi za kumtumia Mwanadamu ili kuthihirisha ufalme wake.
Alimtumia mzee moja wa huko Arusha akawa anatoa kikombe cha dawa ya miti maarufu kama kikombe cha Babu. Huyu naye alikuwa anatumia jina la Yesu. Sasa hivi huyu babu hatumskii tena.
Wako manabii wengi sana wa uongo hapa Tanzania ambao wanatumia Jina la Yesu Kristo.
Yesu Kikristo alisema " watakuja manabii wengi wa uongo na watatoa pepo kwa jina langu"
Ukiona muhubiri anakuwa na Kanisa lake, Mhasibu wa Sadaka ni yeye na mtunza fedha ni mke wake au binti yake ujue hiyo si kutangaza ne no la Mungu ila ni Biashara.
Kwa kifupi Ufalme wa shetani haudumu kamwe na wafuasi wake nao hawadumu kamwe,
Tujiepushe na Manabii wa Uongo.
Serikali izuie Taasisi za Dini za watu Binafsi ambazo hazina mfumo wa Kikanisa na zinakusanya sadaka na kuzitumia kwa maslahi binafsi bila kulipa kodi.