Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Umaskini ni mbaya sana. Huyo mchungaji akamatwe haraka sana.
Kuna mahali wanadamu tumeshindwa kupatumia ktk ubongo wetu, inafika mahali ukisikia kitu huamini unachosikia, mafuta uyakanyage halafu maisha yako yanabadilika kweli?![emoji36][emoji36]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata uchagani wapo kumbe wajinga? Mbona huwa mnasema humu kuwa wachaga wamesoma sana? Au hawakuelimika? Pole zao!
Ndugu kwa hawa wachungaji sijui mtu atachomokaje hata angalikuwa na elimu gani, wanajua sana kusoma madhaifu ya wana nzengo haijalishi kabila wala Elimu gani unayo wao wanatega mitego na lazima unase hasa wakiwa wameshasoma ramani zao vyema.[emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni ndugu zetu God's Plan.
Not GOD's plan... mungu huyo huyo watu wanaemuabudu awaue wakiwa wanamuabudu????? Atakua mkatili kupitiliza.... hapa ni wajinga waliodanganywa mafuta ya upako, wakaanza kuyagombania kwa ujinga wao, wakakanyagana wakauana... usimuingize Mungu kwenye utapeli na ujinga huu
 
Very sad to hear about the loss of lives. May the deceased RIP.

This so called Prophet should be taken to task....
 
We ndo zuzu kweli toka lini Mungu akafanya jambo kwa bahati mbaya. Yaani Mungu aruhusu watu wafe wakiwa kwenye eneo takatifu tena kwa nabii na mtume wake? Huyo ni nabii wa uongo na tapeli.

Mungu mwenyew anasema", Njooni nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha". Kwahiyo hapo ndo kawapumzisha au? Pigo la Mungu huja siku usioizani na siku yake ndo leo. Huko nyuma Mungu alimwacha pengine ili atubu,bahati mbaya akawa jeuri na hayo ndio matunda yake. Bulldozer ni tapeli,na mchawi km ilivyo kwa TB Joshua,Mzee wa upako, Gwajima,Prophet Bushir na Geodavie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata macca hayo mambo hutokea ni kawaida kwenye misingamano hata kwenye viwanja vya soka pia hio ni ajari
 
Sijakuelewa mkuu! Yaani wamekanyagana wakigombea kukanyaga mafuta au wakigombea kuchukua hayo mafuta?

Mungu tuhurumie Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa iko hivi kuna sehemu inaandaliwa watu mnakuwa mnapita mnakanyaga hiyo sehemu huwa na mafuta hayo yaliyoombewa na mtumishi was mungu. Huwa sio sehemu kubwa hapana ni kama upana mita 1 na urefu kama mita 5 . yaani kama ka redcarpert flani hivi mkuu. Sasa tatizo sisi hatuna utaratibu mzuri was kupita kila mmoja anataka kuwa was kwanza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:

Watu 20 (watu wazima 18 na watoto 2) wamepoteza maisha mjini Moshi Kilimanjaro jioni ya leo, baada ya kutokea kukanyagana kwenye kusanyiko la kidini, wakati umati wa watu ukigombea kukanyaga eneo yalipomwagwa mafuta yaliyosemwa kuwa ya upako toka kwa Mhubiri Boniface Mwamposa.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

Chanzo: Mwananchi
Huyu huyu mtu achukuliwe hatua stahiki....

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Back
Top Bottom