Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Sasa hivi Mwamposa ametulia hotelini na mchepuko wake wanahesabu hela huku wachagga wanakodi mahema ya misiba. Kamatahii mutu. Fungia ndani. Ndalichako njoo kuna nwingine huku anahitaji ung'eng'e wako akalale ndani.
[emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi hao waliokufa ni raia wahamiaji kutoka mikoa mingine, mi siamini kama wachaga nao ni wajinga hivyo. ,😂😂😂😂
Kwanza wachaga hawakai mjini mpaka usiku. Wakishafunga maduka yao saa 12 jioni wanapanda zao milimani.
 
Hapa Kuna haja ya kujifunza kwa Kagame lazima wachungaji wawe na kiwango fulani Cha Elimu na sio Kila Mtu kuwa mchungaji kwani bado taifa let Lina kiwango kidogo Cha wasomi ambao wanaweza kung'amua lipi Ni sahihi na lipi sio sahihi, Tafsiri ya vitabu vya dini imekuwa ni changamoto
 
Kwa kukosa maarifa
Sio kusoma maarifa.

Anyway huyo mwamposa ni kijana wa mzee wa upako ila sasa naona kamzidi kete hadi aliye muonyesha janja janja
Ila umaskini ni mbaaaya sana Hawa watu ni matapeli tu sema Imani nayo ngumu hadi mtu akuelewe kuhusu utapeli wao
Asante kwa marekebisho.
Nadhani Ni typing error na nilipost bila kurudia kuangalia nikichokiandika.

Wengi wa Hawa watumishi Ni waongo.
MUNGU ametuagiza kuzijaribu kila roho maana si zote zitokazo kwake.
Lakini huwezi kuzijaribu Kama huna ushirika mzuri na Roho mtakatifu.
Watu wengi hawataki kutengeneza kwanza na Mungu..wanataka utajiri ila hawamtaki Mungu mwenye utajiri
So sad
 
Haieleweki alieturoga Afrika ameenda wapi..unaita mkutano watu wanakuja unawatapeli hela zao na kuwaibia

Katika wizi huo unawapa mafuta feki kabisa nao wajinga wanakanyagana wanakufa halafu unawahi Airpot hata hujali ???

Hivi kweli tuna ujinga kiasi gani sisi????

Huyu Mchungaji tapeli anatakiwa kufunguliwa kesi za kitapeli na kuua watu mpuuzi kabisa.

Lakini na nyie Wachaga kweli ujanja wenu wote huyu tapeli anawaingiza mkenge kweli?? Na hajaja kuwapa hela angalau tuseme mnapenda hela mmezifuata?? Dah
 
Aisee inakuwaje unanitukana, nimekukosea nini, na kama huamini si wewe, inakuwaje unanitukana? Bro tuheshimiane,
Nyongeza_Wewe ni mkumbaff!! Mwamposa ni mungu? Eti wanamkosea mungu!!mtu anasemwa ili aache tabia mbaya ya wizi na ushirikina wewe unasema wanamkosea mungu? Haya sasa tamaa zake zimeshasababisha vifo,ila nasikia amelala sero,angebaki huko hadi angalau keshokutwa apandishwe kizimbani na kuhukumiwa nyundo kadhaa ingependeza zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

Chanzo: Mwananchi
HAYO MAFUTA WANAYOGOMBANIA ETI YANA UPONYAJI WA MARADHI!! SASA CHA AJABU BADALA YA KUONDOA MARADHI YENYEWE YAMELETA UMAUTI.

HEBU WATANZANIA WENZETU EPUKENI MAMBO YA NAMNA HIYO. MNAKUMBUKA MWINGINE ALICHOMA WAUMINI KULE UGANDA? MNAKUMBUKA MWINGINE ALILISHA WAUMINI MAJANI KULE SOUTH AFRICA?

KAMA HAYO MAFUTA YANGEKUWA NA HIZO POWERS YASINGEWALETEA MAAFA WENZETU HAO. DAH

HATUA ZA KISHERIA ZIMESHAANZA NGOJA TUONE MWISHO WAKE.
 
Attachments

  • Screenshot_20200202-092346_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20200202-092346_WhatsApp.jpg
    59.3 KB · Views: 1
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

Chanzo: Mwananchi
Juzi mkurugenzi wa babati mji alianza kufunga makanisa yasiyosajiliwa watanzania hawakumuelewa.sasa huko Moshi watu20 wamekufa kwa uzembe na ujinga wa mtu moja.
 
Watu wetu wamegeuzwa kuwa waabudu viumbe badala ya muumba .Hii ni aina ya shirikina kuamini kitu kitakupa baraka au utukufu fulani alionao mtu utakusaidia wewe, Na hawa wachungaji wapotezaji huwaaminisha watu mambo ili kujikweza wenyewe au kujipatia manufaa ya kipato.
Dini zimegeuzwa DILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni hatari kwa vizazi vijavyo
 
wale wakristo mnisaidiye kuna mahala kwenye biblia yesu aliwapaka mafuta watu,kuuza vitambaa,maji,chumvi na kupokea bahasha zenye pesa?je pia alipofanya miujiza alijitangaza?
Damu ya Yesu, jina la Yesu na neno lake Mungu pekee ndizo silaha tosha kupitia maombi ya kufunga, usiku wa manane na kusali mara kwa mara kwa imani lakini mengineyo yote ni utapeli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom