Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

=====

MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO

Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi

Amesema baada ya hilo tukio wamemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer bila mafanikio. Na kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano

Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, watu wazima 16
ukanyage mafuta wewe gari, na break yenu motoni wapuuzi wakubwa ninyi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kizazi cha ajabu sana hiki, eti hata kuoga tu kawaida kitengenezewe mashine za kuwaogesha, kukuna nazi ni shida pia hadi AZAM Company iwatengenezee chemicalized coconuts za kumimina tu kwenye vyakula sababu ya uvivu tu...[emoji35]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kizazi Cha kusafishwa kucha pumbavu kabisa.Biblia gani imeagiza umwage mafuta watu wakanyage? Hawa ni matapeli wakubwa.ukiambiwa neno upako asilimia 98 ni ushetani tu. Ndiyo maana imeandikwa Msiziamini kila roho Bali mzipime na kuzijaribu muone kama zimetokana na MUNGU.Ukiniambia kukanyaga mafuta.kunywa mafuta najua we tapeli na mwizi tu.
 
Nilicho gundua watu walio wengi humu Jf mnapenda kuongelea vitu kimihemko sana na porojo za kuchangamsha akili kuliko kuongelea uhalisia ambao una ukweli wa kutosha ambao haupendwi wala kusikilizwa na watu wengi wajinga,
Mara nyingi Mwamposa amekuwa akiandaa makongamano ya kukanyaga mafuta Dsm na watu wengi kuponywa na kokote aliko enda halijawahi tokea tatizo lolote iweje Moshi wakati wa kukanyaga mafuta bahati mbaya wengi wakadondoka na kukanyagana, mtu anatokea aliko toka eti "wajinga ndio waliwao" mnamkosea sana Mungu,
Jifunzeni kufanya research vya kutosha kabla ya kutenda wala kuongea lolote, kuna mtu ame-reply eti mafuta ya upako ni kama hirizi tu, na yametajwa hadi kwenye biblia na matumizi yake, Muogopeni Mungu,
Mkuu wewe ndio unaonekana hujui unachoongea au kuchangia. Hakuna bahati mbaya kwenye maisha ya binadamu mwenzio. Ajali zote zinasababu, ma engineer na mafundi tunaamini hivyo. Angalia hata zile movie za final destination, utajua naongea nini.
huwezi weka mafuta sehemu zenye utelezi na population ya watu wengi. Mtu akikanyaga na akakosa balance na kuanguka ina maana atakanyangwa na wenzie. Vilevile huwezi weka container chache za mafuta. Angalia na muda wa hilo tendo coz inaweza ikawa jioni na giza hivyo kila mmoja anataka kuwahi nyumbani au kwingineko.
All in all, hapo kuna uuzembe na ujinga tu.
Acha ujinga mkuu, kama mafuta yanaponya mbona aendi kutoa msaada hospital kwenye wagonjwa hadi anakuja kwetu sisi wazima wa afya na nguvu ya kutafuta pesa? USITETE UPUMBAVU.
 
Wamemkamata dar Alikimbia moshi
Yuko mkononi mwa polisi sahv
Alafu wazir simbachawene amesema Sahv vibanda Imani vimekuwa vingi sanaaaaa[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I am Bless Nabii wenu feki baada ya tukio hilo
Alitoka nduki moshi wamemkamatia dar, Sasa kwann baada ya songombingo huko asibaki
Moshi
Alafu wewe utakuwa ni Wale Waumini mliyowekwa uwanjaa wa ndege kipindi kile mkifanya maombi msafiri kwenda nje bila viza wala ticket..... Mpu gu@n kbsa nyie

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mauaji ya kimbari Rwanda yaliongozwa na mapadri na maaskofu wa kanisa katoliki ambao wote walikuwa na digrii za theolojia.Kagame hajielewi.Yeye mwenyewe huwa anaenda kusali Nigeria kwa TB Joshua ambaye hajawahi somea uchungaji maisha Yale yote
Uongo mtupu huu,Weka picha/video/link kuonyesha Kagame ameemda kusali kwa TB Joshua.

Unadhani huyo ni type za wakina Lowassa/Mwigilu wanaoshinda huko Nigeria kwa huyo Nabii

dodge
 
Mkuu wewe ndio unaonekana hujui unachoongea au kuchangia. Hakuna bahati mbaya kwenye maisha ya binadamu mwenzio. Ajali zote zinasababu, ma engineer na mafundi tunaamini hivyo. Angalia hata zile movie za final destination, utajua naongea nini.
huwezi weka mafuta sehemu zenye utelezi na population ya watu wengi. Mtu akikanyaga na akakosa balance na kuanguka ina maana atakanyangwa na wenzie. Vilevile huwezi weka container chache za mafuta. Angalia na muda wa hilo tendo coz inaweza ikawa jioni na giza hivyo kila mmoja anataka kuwahi nyumbani au kwingineko.
All in all, hapo kuna uuzembe na ujinga tu.
Acha ujinga mkuu, kama mafuta yanaponya mbona aendi kutoa msaada hospital kwenye wagonjwa hadi anakuja kwetu sisi wazima wa afya na nguvu ya kutafuta pesa? USITETE UPUMBAVU.
Asante kaka, Yesu mwenyewe alishughulika na Wagonjwa bila kuwatoza hata Dinari moja, ila huku siye ni mlango wa fursa
 
Utapeli (hila, udanganyifu, kujipatia kipato kwa njia za udanganyifu...)

Kuendesha ibada katika mazingira hatarishi.

Kuhatarisha maisha.

Manslaughter (kuua bila kukusudia).

Kamanda Siro amemtaka ajisalimishe.
Sababu zako hazina mashiko

Utapeli gani Kuna muumini alishaenda kumripoti au alishapata tuhuma hizo ..kwa ushahidi gani ?

Mazingira hatarishi vipi wakati wao ndo walimpa kibali cha mahubiri inamaana kwenye kutoa kibali waliangalia vitu vingi wakajiridhisha wakampa kibali

Manslaughter

Kwani ni yeye kasababisha au uzembe wa watu wenyewe wamekanyagana seriously anahusika vipi hapo



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Macca kila mwaka watu kibao wanakufa hija je nayo ni kafara?
Mbona pamoja na hayo lkn watu hawajawahi kuacha kwenda...
 
Toa neno kdg kamanda
Vp unawaamini Hawa manabii

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu, namuamini Mungu pekee. Zaidi ya Kusali kanisani kwangu KKKT, huwa siendi kwingine popote. Mara moja moja mno huwa nahudhuria semina za Mwakasege. Zaidi ya hapo hapana mkuu.
 
Back
Top Bottom