Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Humu ndani tunasikiaga kuwa wachaga ni waisrael ,wana ufaham na maarifa ya kutosha,ndio wanaoendesha uchumi wa nchi kumbe mburura wakutupwa.Mnauana kwa ajili ya ujinga na upumbavuuu eti mafuta ya baraka kutoka kwa binadam mwenzako.Elimu ni muhim sana katika jamii yetu ya kitanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli nimeamini, kati ya watanzania watatu kuna mmoja ni taira.

yani matatizo yametokea kwenye himaya yake lkn ye anaondoka kama vile hakuna kilichotokea.
na bado waumini wa dar wamempokea na kushiriki nae katika ibada kama hakuna kitu kilicho tokea vile ambacho ni kibaya na kimeumiza hisia za watu wengi.........
hili taifa lina watu wengi vichaa
 
trachomatis,
Let's be honest, umeshawahi kwenda hospital na kuona msongamano wa hao wenye magonjwa uliyoyataja? unajua watu wanachangia kiasi gani kufanyiwa operation za moyo na figo?

kuna watoto wangapi wanapoteza maisha ambao unasema hawana dhambi? kwanini asiende kuwaponya hao badala ya kukimbilia kwa walio wazima wanaotembea barabarani, wenye kutafuta pesa za kujenga na kufanya biashara? sababu ni moja tu, naye anazitafuta hizo pesa.

Tumeona na wengine wanavyonyweshwa sabuni za detto, wanakanyagwa matumbo, kuchezewa uchi na hata kula majani.Je, na hayo wanasingiziwa? vipi kuhusu watu wa Kibwetele? au ulikuwa mtoto bado? walikufa kwa mapenzi ya mungu? Mungu yupi?

points zako bado sana ukilinganisha na madhara yanayotokana na ujinga wa wachungaji wenu.
 
Bukyanagandi,
Sikuelewi kwa hiyo wewe unataka hizo souls 20+ zilizopotea basi ziachwe tu zipotee na maisha yaendelee kama vile hakuna kilichotokea kisha kesho jamaa yako mwamposa aite tena mkutano kama huo achukue tu pesa zake. Na yakitokea maafa tena basi ni ajali. Ajali za kijinga kama hii azipashwi kufumbiwa macho.

Jamaa yako mwamposa inabidi abanwe ili iwe fundisho kwake na wengine waachane na huo wendawazimu wao wanaowafanyia watu kwa mgongo wa miujiza ambayo yote ni fake. Kama ni kuhubiri mtu ahubiri tu na siyo kuja na hayo madawa yao eti watu wakanyage sijui wanywe, nk.

Huo ni ushirikina wa hali ya juu anawafanyia watu. Na siyo haki kufanya hivyo hadi kufikia kuua nyomi ya watu zaidi ya 20!! Oooh God have mercy on your people!!
 
ATOA TAMKO KUHUSU VIFO MOSHI

"Sijafanya mauaji, bali nilikuwa katika kutangaza na kuponya kupitia ufalme wa Mungu. Hakuna kafara pale bali muda wao uliisha na wameitwa na Bwana Yesu watakakoishi milele
[/QUOTE]
Haya maneno kayatamka kweli au ni kujaribu kumlisha maneno kwa vile tayar limeshatokea hili?
Iwapo litakuwa na ukweli huo basi ni dhahiri huyu jamaa anaijua siri ya vifo hivi..😥😥
 
Humu ndani tunasikiaga kuwa wachaga ni waisrael ,wana ufaham na maarifa ya kutosha,ndio wanaoendesha uchumi wa nchi kumbe mburura wakutupwa.Mnauana kwa ajili ya ujinga na upumbavuuu eti mafuta ya baraka kutoka kwa binadam mwenzako.Elimu ni muhim sana katika jamii yetu ya kitanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hawa jamaa wanaojiita manabii wanachuma ulete yao. Wanakamata sana watu hata wenye elimu kubwa tu na hasa ikitokea kukawa na tatizo watu wengi awataki kukubali kwamba changamoto ni sehemu ya maisha yetu. Wanakimbilia kupata tumiujiza bila kujua kuwa huko wanakojipeleka wanaweza kuwa wanajiongezea taabu zaidi kama hizi za kukanyagana, nk.
 
MOS/IR/834/2020 MAUAJI
MNAMO TAREHE 01.02.2020 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO MAJENGO UWANJA WA MPIRA WA MIGUU. KATA YA MAJENGO TARAFA YA MOSHI MASHARIKI WILAYA YA MOSHI NA MKOA WA KILIMANJARO. MTOA TAARIFA NI SP. JOSEPH SALVATORY KATE OCD WILAYA YA MOSHI.

ANAELEZA KUWA ALIBAINI KUUAWA KWA JOYCE TOGORAY CHAMSHAMA MSAMBAA, MIAKA 58, MUUGUZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA HAI MKAZI WA BOMANG'OMBE NA WENZAKE 19 AMBAO HAWAJATAMBULIWA . BAADA YA KUKANYAGWA NA WENZAO WAKATI WANAKIMBILIA KUKANYAGA MAFUTA YA UPAKO YALIYOKUWA YAMEWEKWA GETINI NA ASKOFU BONIPHACE MWAMPOSA BULDOZA NA WENZAKE.

ASKOFU BONIPHACE MWAMPOSA BULDOZA ALIOMBA KIBALI CHA KUFANYA MKUTANO WA INJILI KUANZIA TAREHE 30.01.2020 MPAKA TAREHE 01.02.2020 MKUTANO NI KUANZIA SAA 06:00HRS MPAKA SAA 18:00HRS. LEO ILIKUWA NI SIKU YA MWISHO AMBAPO ASKOFU ALIPITILIZA MUDA NA ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 19:30HRS NDIPO ALIPOWAAMBIA WAUMINI WAKE WAPITE KWENYE MAFUTA YALIYOKUWA YAMEMWAGWA KWENYE TURUBAI GETINI NDIPO YALIPOTOKEA MAAFA.

JUMLA YA WATU ISHIRINI WAMEPOTEZA MAISHA KATI YAO WATOTO 5 WANAWAKE 14 NA MWANAUME 1.

MAJERUHI NI :--
1; GLORY JAMES KISANGA, MCHAGA,MIAKA 16, MWANAFUNZI WA RAU SEC.KIDATO CHA TATU

2;SUZANA MIANGA, MASAI, MIAKA 71, MFUGAJI MKAZI WA NYUMBA YA MUNGU,

3; AGNES LINUS MCHAGA, MIAKA 75, MKULIMA MKAZI WA KIBOSHO KINDI,

4.THOMAS ERABISON MCHAGA, MIAKA 47, MKULIMA MKAZI WA MASAMA,

5; ROZINA STEVEN,

6;MARY MACHA MCHAGA, MIAKA 45, MKULIMA NA MKAZI WA KIBOSHO ROAD,

7; ELIZABETH PETER TARIMO MCHAGA, MIAKA 42, BIASHARA, MKAZI WA MAJENGO,

8; JANETH DANIEL MCHAGA, MIAKA 22.

9; JUNIOR PAULO MMERU,MIAKA 2 NA MIEZI 2,

10: ANJELA SINYANGWA MPARE, MIAKA 36, BIASHARA PASUA,

11: MORIN JULIUS JALUO, MIAKA 24, MKULIMA NA MKAZI WA MERERANI,

12; MARY PAULO MIAKA 23, MUIRAQ, MKULIMA OLD MOSHI,

13; GRACE SHAURI NDERELIO MMERU MIAKA 42, MKAZI WA KIKAVU CHINI,

14; ELIZABETH PETER MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA MAJENGO,

NA WAWILI AMBAO HALI ZAO NI MBAYA HAWAWEZI KUONGEA* JUMLA YAO NI 16.

MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA MAWENZI HOSPITALI KWA UCHUNGUZI WA DAKARI PAMOJA NA NDUGU KUJA KUTAMBUA MIILI YA NDUGU ZAO.

Kiukweli kwenye dunia ya sasa kumekua na matatizo mengi kiasi cha watu kukimbilia kwenye miujiza isiyo na mantiki Mf. Tukio la watu kunyweshwa JICK

Umakini unahitajika kwa wakuu wa madhehebu haya kuhakikisha wana avoid situation yoyote inayoweza kuleta maafa.

Pia umakini mkubwa unahitajika kwa waumini, kuona ni wapi pa kwenda. GOD is omnipresent yupo kila mahali. Popote ulipo ukimuomba anasikia. Hakuna haja ya kukanyaga mafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliomba kibali cha hilo kusanyiko?
Kama hakuomba kibali awekwe ndani na taratibu za kisheria zifuatwe..

Kama aliomba kibali na kupewa basi aachiwe mara moja na jeshi la polisi Moshi liwajibike..
 
Sasa mtume na nabii alipaswa kuwa na mapipa 10 matano amwage nusu ya uwanja mengine waogelee kbsa ,huyu atakuwa kawamwagia Lita moja huyu
 
profftobe,
Unataka kusema nini mkuu! Yaani huna habari kwamba Yesu mwenyewe alikuwa anapunga mapepo, kuponyesha wenye ukoma na magonjwa mengine yaliyo shindikana mpaka anafufua wafu- swali ni, je, Yesu alikuwa anatumia nguvu za giza?

Lugha hizi za kukashfu dini nyingine uchochewa zaidi na Kanisa la Roman Catholic ambalo imani yao ni too rigid hawabadiriki kwendana na wakati - na wasipo badirika na kwenda na wakati, come 40 years from now watakuwa na wahumini wachache sana - to drive point home, nakumbuka kisanga cha Askofu wa dini ya Romani mzaliwa wa Zambia alipo anza kuponyesha watu, kutoa mapepo watu wengi kutoka Nchi mbali mbali walianza kuhudhulia kongamano zake huko Lusaka Zambia watatuliwe shida zao, Papa alipo pata habari zake akampiga marufuku hasiendelee kutoa huduma hizo-just imagine!!

Askofu alipuuza amri ya Papa akaendeleza huduma za uponyaji Lusaka Zambia, Papa alipo pata habari alimlazimisha Askofu kuhamia Roma Italy ili asitishe huduma zake - cha ajabu Askofu aliendelea na hudumazake za uponyaji bila kujali Papa atasema nini, alipo zongwa sana Askofu akakata shauri ya kuoana na mama wa Korea Kusini baada ya kumwarifu Papa, sikumbuki Papa alimjibu nini, lakini Askofu alifunga ndoa na Mkorea eventually na kuhamua kuhamia kwenye dini ya kikristo ya huko Korea - kwa kifupi hapa nataka kuonyesha kwa nini wakristo wengi wanahamua kuhamia kwenye makanisa ambayo yanajali kuwasaidia kutatua matatizo yao yaliyo shindikana na kwa kuwa makanisa hayo haya lazimishi watu kuhama kutoka kwenye imani zao ndio maana utakuta maelfu ya Watanzania wanavutika kuhudhulia kongamano zao bila kusita, kitu ambacho wa Roma pamoja na KKKT hawafanyi labda wabadirike.
 
Pia umakini mkubwa unahitajika kwa waumini, kuona ni wapi pa kwenda. GOD is omnipresent yupo kila mahali. Popote ulipo ukimuomba anasikia. Hakuna haja ya kukanyaga mafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakataa kabisa kabisa wazo lako la kutokuyakanyaga mafuta. Waache wanywe hata hiyo JIK kwa sababu, hiyo ndiyo imani yao. Wadhani ni mara ya kwanza hao watu wameyakanyaga hayo mafuta?? Tuchunguze chanzo ni nini kwanza wala sio kuanza kunyima wasikanyage mafuta.
Mimi sikanyagi mafuta kwa sababu;
1. Mafuta niliambiwa nitamiminiwa kichwani yatiririke nami ili popote nikipita myone mjue nilipoelekea. Sijaambiwa niyakanyage.
2. Sijui ni nini kazi ya hayo mafuta. Nahitaji UPAKO kwa kazi maalum, hapo sijui ilikuwa kazi gani
Nadhani watu wamechukulia haya mafuta ka hirizi flan hivi. Hili sio zuri
 
Jamii ya kiafrika inasumbuka na kukosa maarifa.

Kwa wafrika maisha ni pesa.

Suala la pesa ni nini, inatoka wapi, na inapatikaje, hayo maarifa hayapo kwa mwafrika.

Mwafrika anatumia njia yoyote bila kutazama uharibifu au madhara yatokanayo na njia au jambo au kitu hicho kiakili na kimwili akitaka tu pesa au mamlaka au sifa.

Ni kukosa maarifa !

Inawezekanaje mtu akakwambia yeye ni nabii au mwalimu au mtume, kwa mfano halafu ukamkubalia usiulize hayo mamlaka ameyatoa au amepewa nani ?

Mtu anakuja anawambia ana uwezo wa kuponya au ana mafuta ya kuponya au sijui ana hiki kinakufanya uwe tajiri, usiulize hayo mamlaka ameyatoa au amepewa na nani ?

Mwaka 2012 alitokea mtu mmoja huko Mkoani Arusha akadai ameoteshwa na Mungu dawa ya kuponya HIV/AIDS na maradhi mengine sugu. Tuliona watu walivyoenda na tunajua matokeo yake yalivyokuwa.

Tuwaelimishe watu wetu hasa akina mama, wanawake dhidi ya hawa wahuni, wazushi, waongo na matapeli wa dunia hii.

Watu wengi wanasumbuka na matatizo ya kisaikolojia, shinikizo la damu na hali duni ya maisha. Matatizo haya yana chanzo chake katika ndoa au mapenzi na makosa dhidi ya akili.

Watu wameacha mafundisho sahihi,dini ya kweli: wameacha Sakramenti wamefuata vikanisa na mafundisho potofu, mafundisho ya uongo na mazingaombwe ya miujiza.
 
Back
Top Bottom