Nimefikiria sn kuhusiana na usalama wa hili taifa letu nikaona hii Amani tuliyo nayo imetulevya kiasi sasa tunelewa hatujitambui na tunalala milango wazi Mali zetu za ndani hazina ulinzi tena.
Kilicho nisukuma kuandika Uzi huu ni tukio la juzi la kukamatwa kwa wahamiaji haramu 81 wakiwa porini wamejificha.
Wengine wakahusishwa na maiti za watu 6 waliotupwa ndani ya mto Ruvu hivyo idadi yao ikafikia jumla ya watu 87.
Nikaanza kujuuliza Kama idadi ya watu hao 87 wakiwa na uwezo wa kupambana kivita sawa na wale MAKOMANDOO wetu wa siku ile ya sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika tutapona kweli?
Ajabu waziri wa mambo ya ndani hadi Leo hii hajatoa kauli yoyote Kali ya kuwakemea Askari wake kwa uzembe huu . Polisi wengi wapo bize na kukusanya mapato ya barabarani na kutangaza faida waliyopata kila mwezi huku wakiacha mipaka yetu ikiwa wazi.
Tujiulize wanapitaje hawa watu humu barabarani kwa jinsi polisi walivyo kuwa wengi na vizuizi vyao?
Polisi badala afanye ukaguzi wa gari zima kwa samplerin utaona anaenda kunong,ona na dereva akipewa chake anaruhusu gari kuondoka kumbe roli zima limejaa Wasomali na Waethiopia badala ya mizigo.
Mara kwa Mara polisi tunasikia wameuwawa na kuporwa bunduki,, hii yote ni sababu ya kuacha kutekeleza majukumu ya Kazi yao wanafanya ya TRA.
Hivi hao watu Kama waliweza kuingia nchini kwa idadi Kubwa hivi wakiamua kuhujumu Maji yetu kwa sumu ,, ni watanzania wangapi watapoteza uhai wao.
Siamini hata kidogo hivi kweli mtandao huu wa kuvusha hawa wahamiaji haramu ni mkubwa kuliko ule wa madawa ya kulevya au kuzidi ule wa kuiba makontena pale bandarini ambayo yote imedhibitiwa sasa hv .
Mh. Mwigulu Nchemba hebu amka ndg yngu watumbue wewe kabla JPM hajakutumbua wewe.