Motivation Speaker anatakiwa awe Ally Hapi, Siyo wale kuongea pasi vitendo

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Huyu jamaa ameamua hasa, japo tayari ameingia akiwa na mtaji ila huyu ndiye motivation speaker ambaye anatakiwa kuongea akiwa anamaanisha, siyo yule/wale wa hekari moja unapata 12mil.

20230316_203319.jpg

Anachifanya huyu kijana Ally aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara huko kwenye mashamba yake ni mfano tosha kwa vijana kama wale ambao mh. Waziri wa kilimo Hussein Bashe anawaunganisha na kuwapa hatishamba kwa kuanza kilimo.
20230316_203520.jpg

Nimefuatilia kwenye ukurasa wake wa tweeter kuangalia mwitikio wa watu wanao_comment kwenye tweet zake wengi wanamsifu na kuvutiwa na kile anachokifanya, hata wale mahasimu wake hawaonekani ila ukichungulia nyuma unawaona wanapita kimya kimya.

20230316_203356.jpg

Hadi hapo maswali na majibu yanapatikana labda sababu iwe ni capital a.k.a mlungula wa kuwekeza, maana kufanya anachokifanya huyu motivation speaker Ally Hapi siyo unaamka na mkopo wako ukidhani mwezi ujao unaanza kuvuna.

Ni yataka moyo kweli kweli.
 
Wale mnaopata airtime kwenye media na kuanza kudanganya wananchi kuwa, ukilima nusu heka unapata milioni 9 au kuku mmoja anataga mayai 24 ukiwa na kuku 3 unapata mayai 72, yakitotolewa unakuwa na vifaranga 72.

Wakikua kila kuku unauza shs 20,000 jumla utakuwa na shs 1,440,000/-, ingia field sasa 😀!.
 
Safi sana ,hapo chini ni analima na mpunga pia? Nimeona Alikiba analima nyanya pia
Hivi hawaibi?au anaweka walinzi

Ally Hapi alipoingia Iringa alijenga kwanza nyumba ya kuishi, akanunua mashamba makubwa sana , hata alipohamishiwa tabora kisha mara bado wafanyakazi walikuepo shambani na msimu ule wa kwanza akiwa Iringa nyanya ilikubali akakutana na soko akagonga kama milioni 45, ndio toka hapo hakuacha, tunapuuzia kilimo lakini ukiwa na mtaji unatoka, kuna jamaa mmoja wa TRA songea yeye kule peke yake hua anavuna gunia za mahindi hadi 5000 akianza kuuza mnanunua hadi mnakimbia wenyewe ana trekta kama 5 hivi massey ambazo wakati anaanza alichukua zile used za msumbiji, “ kama unataka mali utayapata shambani “
 
Sure
 
Ni kweli kabisa usemavyo hawakukosea mali utaipata shambani
 
Back
Top Bottom