Huyu jamaa ameamua hasa, japo tayari ameingia akiwa na mtaji ila huyu ndiye motivation speaker ambaye anatakiwa kuongea akiwa anamaanisha, siyo yule/wale wa hekari moja unapata 12mil.
View attachment 2554157
Anachifanya huyu kijana Ally aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara huko kwenye mashamba yake ni mfano tosha kwa vijana kama wale ambao mh. Waziri wa kilimo Hussein Bashe anawaunganisha na kuwapa hatishamba kwa kuanza kilimo.
View attachment 2554161
Nimefuatilia kwenye ukurasa wake wa tweeter kuangalia mwitikio wa watu wanao_comment kwenye tweet zake wengi wanamsifu na kuvutiwa na kile anachokifanya, hata wale mahasimu wake hawaonekani ila ukichungulia nyuma unawaona wanapita kimya kimya.
View attachment 2554166
Hadi hapo maswali na majibu yanapatikana labda sababu iwe ni capital a.k.a mlungula wa kuwekeza, maana kufanya anachokifanya huyu motivation speaker Ally Hapi siyo unaamka na mkopo wako ukidhani mwezi ujao unaanza kuvuna.
Ni yataka moyo kweli kweli.