Moto katika baridi kali

Moto katika baridi kali

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2014
Posts
460
Reaction score
285
Wana Jukwaa salaam. Napenda kujuzwa, ni nini huwa kinasababisha moto kuwaka kwenye ile misitu ya nchi za magharibi (Marekani na Urusi) kwa mfano hasa kipindi cha baridi kali? Nijuavyo mimi dawa ya moto kuzimwa ni maji, sasa ule moto unaozuka na kusababisha hasara kubwa, tena unaunguza hata miti iliyo na ukungu wa barafu, huwa ni moto wa aina gani? Tena huwa nasikia na nilisoma mahala ya kuwa, huwa unazimwa kwa maji maalumu yenye dawa maalumu.

Naomba kuwasilisha.

Ahsante!
 
Kinachoufanya moto uwake ni hewa na maji yakuzimia moto duniani kote huwa na dawa maalum hata hapa bongo ni hivo hivo.
 
Moto Ili uwake unahitaji vitu 3...1.Oxygen (Na sio hewa tu coz hata Carbon dioxide Ni hewa)...2.Kilipuzi (Baruti, Sigara yenye Moto, Kiberiti n.k)....3.Kisambazaji (Mafuta, Karatasi, Miti, Nguo n.k)......Ukiondoa kimoja katika hivyo 3 hapo juu, hakuna Moto!
 
kuna sababu kuu mbili ambazo zinasababisha forest fire,ya kwanza, ni sababu za kibinadamu(human cause)na ya pili ni sababu za asili(natural cause)lakini human cause hazina madhara makubwa kwasababu ni rahisi sana kuzuilika kuliko natural cause ambazo zina madhara makubwa(japo kuwa ni 12% tu ya chazo)..upande wa natural causes,moto unaweza kusababishwa aidha na radi au mlipuko wa volkano(volcanic eruption),kama ulivyoelezwa hapo juu moto unategemea vitu vikuu vitatu oxygen,joto,na fuel(miti),radi hizi zinazosababisha huu moto mara nyingi huwa haziambatani na mvua na hupiga mara 100 kwa kila sekunde..sasa ipo hivi kwenye msitu kuna oxygen(1),pia kuna miti/fuel(2) lakini hakuna joto/heat(3)..kwahiyo volkano itakapo lipuka(erupt) au radi itakapo piga lazima itatengeneza "spark" ambazo ndizo zinazo sababisha joto(3)..hivyo basi vitu vyote ambavyo ni muhimu ili moto uwake yaani oxygen,fuel, pamoja na joto vitakuwepo na mwisho moto utawaka tu!
 
Canada pekee, 45% ya mioto ya misituni inasababishwa na radi/lightning na mioto hii inapelekea 81% ya madhara ya mioto yote. 55% ni sababu za kibanadamu na mioto hii ni rahisi kuzuilika kuliko ile inayosababishwa na lightning.
 
Nawashukuru wote kwa maelezo mazuri, tena ya kitaalamu zaidi, nasubiria wajuzi zaidi watufafanulie hili, huwa linanitatiza sana kwa kweli yaani unaona taarifa ya moto kwenye misitu na ndege zinapita juu kumwaga maji sijui dawa za kuuzima, ila ukiangalia vizuri hiyo miti, unaona kabisa ina ukungu ama mabaki ya barafu, kwa sababu ya baridi kali, yaani napata ukakasi kweli kwa hili. Endeleeni kutuelimisha jamani.

Ahsante!
 
Nakushuuru sana.

Ahsante!

Canada pekee, 45% ya mioto ya misituni inasababishwa na radi/lightning na mioto hii inapelekea 81% ya madhara ya mioto yote. 55% ni sababu za kibanadamu na mioto hii ni rahisi kuzuilika kuliko ile inayosababishwa na lightning.
 
Shukurani mkuu.

Ahsante!

Moto Ili uwake unahitaji vitu 3...1.Oxygen (Na sio hewa tu coz hata Carbon dioxide Ni hewa)...2.Kilipuzi (Baruti, Sigara yenye Moto, Kiberiti n.k)....3.Kisambazaji (Mafuta, Karatasi, Miti, Nguo n.k)......Ukiondoa kimoja katika hivyo 3 hapo juu, hakuna Moto!
 
Ubarikiwe sana kwa elimu hii uliyoitoa.

Ahsante!

kuna sababu kuu mbili ambazo zinasababisha forest fire,ya kwanza, ni sababu za kibinadamu(human cause)na ya pili ni sababu za asili(natural cause)lakini human cause hazina madhara makubwa kwasababu ni rahisi sana kuzuilika kuliko natural cause ambazo zina madhara makubwa(japo kuwa ni 12% tu ya chazo)..upande wa natural causes,moto unaweza kusababishwa aidha na radi au mlipuko wa volkano(volcanic eruption),kama ulivyoelezwa hapo juu moto unategemea vitu vikuu vitatu oxygen,joto,na fuel(miti),radi hizi zinazosababisha huu moto mara nyingi huwa haziambatani na mvua na hupiga mara 100 kwa kila sekunde..sasa ipo hivi kwenye msitu kuna oxygen(1),pia kuna miti/fuel(2) lakini hakuna joto/heat(3)..kwahiyo volkano itakapo lipuka(erupt) au radi itakapo piga lazima itatengeneza "spark" ambazo ndizo zinazo sababisha joto(3)..hivyo basi vitu vyote ambavyo ni muhimu ili moto uwake yaani oxygen,fuel, pamoja na joto vitakuwepo na mwisho moto utawaka tu!
 
Mara nyingi hutokea wakati wa summer (majira ya kiangazi), sijawahi kuona misitu iliyojaa barafu ikiwaka moto kirahisi hivyo....
 
Ndugu, fuatilia na ipo siku utakuja kulishuhudia hili. Japo nashukuru wenzio hapo juu wameelezea kwa kina na wao naamini walishashuhudia hili. Utakuja kuona ama kusikia tu siku moja, wala usitie shaka.

Back
Top Bottom