Moto Mkubwa unawatesa Wamarekani wa Jimbo la California

Moto Mkubwa unawatesa Wamarekani wa Jimbo la California

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Tizama dunia hii. James Woods, muigizaji maarufu wa Hollywood ambaye alishabikia Wapalestina wote wa Ghazza wateketezwe, Mungu kamtahini kwa kuunguliwa na nyumba yake katika moto mkubwa unaoendelea kuiteketeza California, sasa analia kama mtoto mdogo! Ama kweli mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi


















1736752021019.png



1736772798427.png
 
Mungu hausiki na haya majangaz pia what if sio karma ni mipango ya watu wachache ili kupush agenda zao kwa serikali?
Mungu anaweza kuwatumia viumbe wake kulipa kisasi ulitaka Mungu mwenyewe aje kuwasha moto na watu wamuone ndipo utakapo amini kazi ya Mungu?Mungu ana njia nyingi za kuweza kuwaadhibu watu wabaya kwa njia zozozte zile.
 
Mungu anataka kulihamishia Jua Duniani tuchomeke. Jehanam ni JUA, maana huo ndio moto unaowaka bila kukoma, na ndiko wale wenyedhambi wanaosemwa kwenye biblia watachomeka huko.

Ila huko Los Angeles wamezidi uovu, sasa Mungu kawaletea Jehanam hapo hapo kwao, moto unawaka hauzimiki mpaka waishe.
 
Sababu ingekuwa ni Gaza huo moto ungeanzia Israel. Huo moto ni janga kama majanga mengine wala siyo karma kwa Marekani kufadhili vita vya Gaza au Ukraine.
 
Nimetafakari sana, Wamarekani wanaojiona wana kila kitu wameshindwa kujiokoa kwenye hili janga… Ndivyo wale watoto wasio na hatia Gaza wanavyoshindwa kujiokoa!
Mkuu hao jamaa wanajitahidi sana ukilinganisha ukubwa wa janga, casualties na muda wanaotumia. Huo moto una ukubwa wa nusu ya eneo lote la mkoa wa Arusha.
Kuna ule wa mwaka jana Texas ulikuwa na ukubwa mara 3 ya eneo lote la mkoa wa Dar na walitumia kama siku 19 kuudhibiti.

Sasa imagine janga ukubwa kama huo litokee hapa bongo tena eneo lenye makazi ya watu sio porini kama ule wa mlima Kilimanjaro.
 
Sababu ingekuwa ni Gaza huo moto ungeanzia Israel. Huo moto ni janga kama majanga mengine wala siyo karma kwa Marekani kufadhili vita vya Gaza au Ukraine.
Usichojua ni marekani ndio inapigana uko Palestine iyo Israel ni kiini macho tu wajeda silaha zote za marekani yeye ndio mwenye vita yake,
 
Watumie mbinu ya kuchimba kama barabara kati ya eneo lenye moto na lisilo na moto kutenganisha mawasiliano vinginevyo maji wataita mma
 
Haya majanga yapo tu siku zote na yataendelea kuwepo milele na wala hayana mahusiano yoyote na mambo ya Gaza kwani hata huko Gaza Israel hakukurupuka tu na kuanza kuishambulia Gaza.

Ila watu wenye kufagilia tamaduni za wengine wakiona hayo ndio wanapata mtaji wa kueneza propaganda za uongo.

Nakumbuka mwaka 1974 tulipata njaa ya kihistoria hadi Mwalimu Nyerere ilibidi aende kuomba msaada wa chakula nchini Marekani na kupewa tani na tani za mahindi ya njano yaliyobatizwa jina la Yanga pamoja na Bulgar na ndipo watanzania tukapumua, sasa kwa hilo janga sisi tulikuwa tunapewa adhabu ya nini...!!??😲😲😲
 
Back
Top Bottom