Haya majanga yapo tu siku zote na yataendelea kuwepo milele na wala hayana mahusiano yoyote na mambo ya Gaza kwani hata huko Gaza Israel hakukurupuka tu na kuanza kuishambulia Gaza.
Ila watu wenye kufagilia tamaduni za wengine wakiona hayo ndio wanapata mtaji wa kueneza propaganda za uongo.
Nakumbuka mwaka 1974 tulipata njaa ya kihistoria hadi Mwalimu Nyerere ilibidi aende kuomba msaada wa chakula nchini Marekani na kupewa tani na tani za mahindi ya njano yaliyobatizwa jina la Yanga pamoja na Bulgar na ndipo watanzania tukapumua, sasa kwa hilo janga sisi tulikuwa tunapewa adhabu ya nini...!!??😲😲😲