Moto wateketeza ghala lenye mizigo ya magendo na waliokwepa ushuru Tanga

Moto wateketeza ghala lenye mizigo ya magendo na waliokwepa ushuru Tanga

Nimeshtuka na hii habari sana mbona kama inafikirisha
Si vitenge vilitoroshwa mkuu wa mkoa akatoa adhabu sasa hivi vikivyoungua vilikuwepo tena ?
 
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa Omary Mgumba, ghala lilikuwa na mizigo ya Mamlaka ya Mapato (TRA) ikiwemo Vitenge vilivyokamatwa kwa Magendo baro 370 pamoja na Sukari, Mafuta ya Kula, Baiskeli na Pikipiki

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa, Fatuma Ngenya amesema wamefanikiwa kuudhibiti Moto ulianza saa 8 usiku eneo hilo na uchunguzi wa chanzo chake umeanza.

==================

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika umezuka usiku wa kuamkia leo kwenye ghala la Bandari ya Tanga ambalo lilikuwa limehifadhi mizigo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga vikiwemo vitenge vya magendo baro 370, sukari, mafuta ya kupikia, pikipiki na baiskeli ambavyo ni mali ya Wafanyabiashara ambao wameshindwa kulipia ushuru na vyote vimeteketea kwa moto.

Mkuu wa wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amezungumza leo asubuhi wakati moto ukiendelea kuzimwa ambapo amesema tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku ambapo ghala hilo lilikuwa linahifadhi vitu mbalimbali vya magendo ikiwemo mizigo ya walioshindwa kulipa ushuru.

Mgumba amesema, hadi sasa mkazo wao mkubwa ni kuhakikisha moto unazimwa kabla ya uchunguzi kuanza ili kubaini chanzo cha moto huo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Tanga, Fatuma Ngenya amesema hadi sasa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo.
Tanga ni kuchafu sana kwa Rushwa! Watumishi wengi Tanga wananuka Rushwa! Serekali Kuu naiomba iitupie jicho la tatu hapo Tanga!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Muda wa kutoa report itakua kimya kimya na hata lisisikike Jambo lolote kwani hiyo ni inside Job! Hujuma au arson
 
Back
Top Bottom