Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Moto ambao bado chanzo chake hakijafahamika umeunguza vibanda vya wafanyabiashara zaidi ya 30 katika soko la mbao Sabasaba Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Akithibitisha kutokea tukio hilo leo Jumatatu Machi 17, 2025, Kaimu Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, Elisa Kamugisha amesema moto huo ulianza saa 7 usiku.
Amesema soko hilo linakadiriwa kuwa na wafanyabiashara zaidi ya 1,000 lakini walioathirika na moto huo ambao chanzo hakijafahamika ni wafanyabiashara 30.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameagiza uchunguzi ufanyike ili kujua chanzo cha moto huo huku akiwataka waathirika kuwa watulivu wakati hatua zaidi zikiendelea.