mottor and dynamo kwa umeme wa bure

Binafsi nilijaribu, nikakwama. Nilikuwa na battery ya gari, inverter, dynamo ya Volkswagen (inayotumika badala ya Aultenata); motor. Nilichobain ni kwamba dynamo ili ifue umeme,na inapofua huo umeme inahitaji nguvu sana kuisukuma/kuizungusha. Mottor za kawaida haziwezi kuizungusha hiyo dynamo. Hapo nikakwama.
Umeme ulitoka kwenye battery (12V DC), inverter ikabadili umeme huo kuwa 220V AC. Umeme huo ukaizungusha mottor, mottor iizungushe dynamo. Dynamo itoe umeme kuchaji battery, na battery ipeleke ummeme (12V DC) kwenye inverter.

Mambo yakawa mazito. zoezi likashindwa.
 
Mada hii imekaa vizuri, kupata umeme wa gharama ndogo hapo tunahitaji support ya serikali, mfano China Solar Valley. Wanatumia Solar, biogas na wind energy tu mji mzima. Lakini project imefadhiliwa na government. Pia vyuo kufundisha solar and other renewable energy source related courses. but kwa hilo wazo hapo juu its impossible
 

WAZO JiPya: "Inawezekana". Kwa kutumia maji inawezekana, Norway wamejaribu. Inabidi uwe na chanzo cha maji. Mfano, maji yanakuwa kwenye bwawa kwenye mwinuko. Unayatega kwa kutumia simple technology (mfano, jinsi miji ya kale ilivyopata maji kutoka bondeni kwenda kilimani kwenye mji-miaka kadhaa BC). maji hayo yataendesha turbine ambayo itafua umeme. Umeme utatumika nyumbani na kuendesha pampu itayosukuma maji kurudi kileleni. Hapo mzunguko utaendelea. Nota Bene: Utafuga na samaki pia bata kwa kuwa maji unayo.
 
WAZO JiPya: "Inawezekana". Kwa kutumia maji inawezekana, Norway wamejaribu. Inabidi uwe na chanzo cha maji. Mfano, maji yanakuwa uwe na bata kwani maji utakuwa nayo.
mkuu ili maji yaweze kufanya kazi yanahitaji force; na hii force inategemea kina macho yanapotoka;

which brings us to Pressure = Height (kina) x Density (ya hayo maji) x Gravitational Force

Sasa utaona kwamba ili hayo maji yafanye kazi inabidi tuyapandishe juu (height) na kuweza kuyapandisha juu tunahitaji force iwe ni pump au tuyabebe kwa ndoo...

Na utaona kwamba nguvu tutakazozitumia kuyapandisha juu ni kubwa kuliko umeme tutakaopata.. (hivyo ndio maana huwa tunangoja mvua zinyeshe ili zitusaidia kujaza hayo mabwana ambayo kuna kina kirefu
 
M.L. unachoongelea ni sawa na mabwawa yetu haya kama Hale na Mtera,zote mechanism ziko hivyo,nilikuwa namaanisha kusiwe na kitu kingine hapo katikati,yaani dynamo na motor tu,na hiyo motor itoe umeme from the dynamo....tuendelee kuumiza vichwa
 
Last edited by a moderator:
Aisee,nimewahi kufikiria hii kitu enzi hizo nikiwa o-level,yaani ilini-irritate sana basi tu nikaamua kuipotezea!
 
M.L. unachoongelea ni sawa na mabwawa yetu haya kama Hale na Mtera,zote mechanism ziko hivyo,nilikuwa namaanisha kusiwe na kitu kingine hapo katikati,yaani dynamo na motor tu,na hiyo motor itoe umeme from the dynamo....tuendelee kuumiza vichwa

Sawa, ila ni jambo gumu. Hakuna umeme chini ya KV13 ambao utaweza kuendesha dynamo ya kufua umeme. Ili dynamo ifue umeme wa 12V DC yenye current kubwa lazima mashine inayoizungusha dynamo hiyo iwe na HousePower kubwa.
Kwa mantiki hiyo, pana ugumu. Vinginevyo umeme huo ungekuwepo.
 

Excellent explanations....
 
Concept kama hizi zimekuwepo toka enzi na enzi. Google perpetual energy. Utaona cases tofauti tofauti ambazo watu wamejaribu kufanya na ikashindikana.

Hii feedback mechanism unayoiongelea pia ilisha jaribiwa.
 
Guys msiwakatishe tamaa watu. science grow through other men critisism. mimi niko kwenye project yangu ya kutengeneza umeme na nimefanikiwa ninakusanya vifaa ili niweze kutengeneza kitu kikubwa sasa. nimetumia sumaku 4 za hard disk nikazifunga kwenye feni ya cpu inazunguka kwa miezi 4 sasa na haijawahi kupunguza speed na ninafurahia coz kwa sasa nataka kutengeneza feni isiyotummia umeme na baadae nitatengeneza motor kubwa itakayyowasha umeme nyumbasni kwangu
 
kama umeweza kuwa na dynamo nakushauri ujaribu umeme wa uupepo,siyo ule wa mnara mrefu utakugharimu ku erect mnara,nazungumzia ule wa kutumia pipa lililokatwa kwa urefu nakutegwa kuwa turbine ambayo ikipigwa na upepo inazungusha dynamo ambayo itafua umeme kwa ajili ya kuchaji betri . Ukiwa interested Hebu Google "vertical wind turbine" upate maelezo kwa kuna.
 
VP mkuu hii project yako umefanikiwa?
 
 
Inawezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…